Kredity

PERFORMING ARTISTS
Komando Wa Yesu
Komando Wa Yesu
Performer
COMPOSITION & LYRICS
YAMUNGUMENGI ZADOCK KINYENZI
YAMUNGUMENGI ZADOCK KINYENZI
Songwriter

Texty

[Verse 1]
Mtakaa asubuhi, kiza kitaingia
Kusubiri aibu yangu kama mlivyozoea
Ina maana hamjui, imebaki historia
[Verse 2]
Kati ya watakaofutwa machozi, nami nimechaguliwa
Kilio changu cha muda mrefu, amekisikia
Hakuna tena cha mikosi: ni kufanikiwa
[Chorus]
Wa zamani si wa sasa
Mambo yamebadilika, eh
Imekula kwe - imekula kwenu eh
[Verse 3]
Namjua ninayemtumikia
Namjua ninayemwimbia
Mfalme wa wafalme, funguo ya maisha yangu
Mlinicheka sana, mpaka kudiriki kusema
Namwamini Mungu, asiyeona
[Verse 4]
Na niliposema nitajenga majumba, yaani, mlicheka sana
Niliposema nitamiliki magari, mkaguna "mhh, ndoto ya mchana"
Mkasema ni ndoto, ndoto, niache utoto
Maana haiwezekani
[Verse 5]
Kumbe yupo Msemaji wa mwisho
Anaandaa kesho yangu
Nisibakie kama jana, aibu hiyo
[Refrain]
Baba yangu si kiziwi hata asinisikie
Baba yangu si kipofu hata asinione
Baba yangu si mchoyo hata asinibariki
Mlipanga mabaya imekula kwenu
[Verse 6]
Wa zamani si wa sasa
Mambo yamebadilika
Mlipanga nife, imekula kwenu, eh
[Chorus]
Wa zamani si wa sasa
Mambo yamebadilika
Imekula kwe - imekula kwenu eh
[Verse 7]
Wa zamani si wa sasa
Yale yaliyonitesa
Nayo yamebadilika, imekula kwenu, eh
[Chorus]
Wa zamani si wa sasa
Mambo yamebadilika, eh
Imekula kwe - imekula kwenu eh
[Verse 8]
Walizoea kuona naharibikiwa
Wakasema sitafanikiwa
Mungu, amebadilisha mambo
[Verse 9]
Pale akili yenu ilipoishia
Baba yangu nd'o anapoanzia
Jambo, kufanya jambo
[Verse 10]
Mtakaa barazani kuniongelea
Mabaya kuniombea
Ila ng'ambo, nitavuka ng'ambo
[Verse 11]
Kama ni kiwete nimetembea
Aibu kaniondolea
Mimi sio yule wa jana
[Chorus]
Wa zamani si wa sasa
Mambo yamebadilika, eh
Imekula kwe - imekula kwenu eh
[Chorus]
Wa zamani si wa sasa
Mambo yamebadilika, eh
Imekula kwe
[Verse 12]
Tunaye Baba mwenye uweza, Alfa na Omega
Huinua wanyonge toka mavumbini machoni pa adui
Unayenisikiliza, kipi kinakuliza?
Mwambie Yesu, achana na wanadamu hao
[Refrain]
Hata wakuite tasa, sawa
Waseme masikini, sawa
Waseme huolewi
Matusi yote wamalize
[Refrain]
Wala usiwajibu, sawa
Nyamaza kimya, sawa
Kisasi si chako wewe
Mambo yatabadilika
[Chorus]
Wa zamani si wa sasa
Mambo yamebadilika, eh
Imekula kwe - imekula kwenu eh
[Chorus]
Wa zamani si wa sasa
Mambo yamebadilika, eh
Imekula kwe - imekula kwenu eh
[Refrain]
Mimi si yule wa jana, wa sasa
Namuona Bwana, badilika
Usiku na mchana
Imekula kwenu, imekula kwenu
[Refrain]
Yaliyoshindikana, wa sasa
Yamewezekana
Hata useme hapana
Imekula kwenu, imekula kwenu eh
[Outro]
Wa zamani si wa sasa
Mambo yamebadilika, eh
Imekula kwe - imekula kwenu eh
Written by: YAMUNGUMENGI ZADOCK KINYENZI
instagramSharePathic_arrow_out

Loading...