Musikvideo

Darassa Ft. Winnie - Nishike Mkono (Official Video)
Schau dir das Musikvideo zu {trackName} von {artistName} an

Credits

PERFORMING ARTISTS
Darassa
Darassa
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Darassa
Darassa
Songwriter

Songtexte

Nobody see me crying All I know is nobody by my side Mungu nishike mkono Nishike mkono (nishike mkono) Nishike mkono (nishike mkono) Nishike mkono (nishike mkono mkonoo) Mwili kama una vidonda ukinigusa tu naumia Kichwani mizigo ya dhambi gunia kwa magunia Dunia sinia pakua unachoweza Nirudishe kwenye njia walimwengu walishanipoteza Mpaka leo bado mwanangu yupo magereza Mtoto wa jirani anasomeshwa uingereza Babaake na Athumani alikufa mvuvi wa pweza Mwenye utajiri wa imani masikini wa kifedha Washanichimbia kaburi wanizike nahema Washakata miti ya vivuli mifereji ya neema Unaweza kuta unaemuamini ndio anaekuwekea sumu Hawana alama binadamu anaekuja kukuhukumu Mwili umechoka naforce tu kuendelea Mpaka naogopa wapi naenda kutokea Hata nikiokoka nani ataniletea Nisipotoka maisha yananitokea damn Nobody see me crying all I know nobody's by my side Mungu nishike mkono Nishike mkono (nishike mkono) Nishike mkono (nishike mkono) Nishike mkono (nishike mkono mkonoo) Kumekucha nipo njia panda sioni hata pa kuelekea Na kiza ndio kinatanda niendako nani wa kunipokea Nishike mkono (nishike mkono) Nishike mkono (nishike mkono) Nishike mkono (nishike mkono mkonooo) Unajikuta uko peke yako giza kubwa kwenye mtaa Huoni ndugu wala jamaa uliokuwa nao jana bar Mawazo ya karaha nafsi inakosa raha Upepo mkali na baridi bila koti la kuvaa Unajiuliza Mungu where you are uoneshe njia Kelele za uchungu na hakuna anaekusikia Usitamani kiatu changu we ukivaa hautembei Ikiwa ni siku mbaya ndio masaa hayasogei damn Nobody see me crying all I know is nobody by my side Mungu nishike mkono Nishike mkono (nishike mkono) Nishike mkono (nishike mkono) Nishike mkono (nishike mkonoooo) Ayoo imagine maisha ya mtoto bila mzazi wa kumlea Nambie ndoto za wangapi mitaani zimepotea Imagine mzazi wa lulu maumivu aliyojibebea Sometimes tunaishi nje ya malengo tuliyojiwekea Kifuani kama kuna moto Moyo wangu unaungua Maumivu nnayopata usitamani kuyajua Nashindwa kupiga hatua uwoga nasuasua Maji yakiwa shingoni ndio nakumbukaga dua Nashindwa kuchagua kati ya mvua na jua Kuna kitu kinamiss nawaza kukigundua Natamani kuwa mtoto kibaya haiwezi kuwa Vazi la dhambi nililovaa halitakati hata nikifua Mwili umechoka naforce tu kuendelea Mpaka naogopa wapi naenda kutokea Hata nikiokoka nani atakaeniletea Nisipotoka maisha yananitokea Nobody see me crying all I know is nobody by my side Mungu nishike mkono×2 Nishike mkono (nishike mkono) Nishike mkono (nishike mkono) Nishike mkono (nishike mkono)
Writer(s): Ramadhani Thabit Shariff, Winifrida Mmasi, Gardson George Sakaya Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out