Στίχοι

Vipeperushi vinasambaa Eti natafutwa Nimepotea wiki imekataa Ndugu wamechachamaa Wananitafuta Nimepotea mwezi umekata Kazini sionekani, yupo wapi huyu Simuni sipatikani, yupo wapi huyu Baba kaniulizia, yupo wapi huyu Mama aishi kulia, yupo wapi huyu mimi Nimezama katika kina kirefu Cha bahari ya mapenzi Nimezama katika kina kirefu Cha bahari ya mapenzi Sio ya Andit Purre mwana Rajab mlomkuta Tanga Sijafanywa msukule msipate tabu kumaliza waganga Amenirudisha shule hesabu maumbo kupanga Penzi la wasasambule lenye protini, vitamin na wanga Aaaah! ladha yake, si sukari Ni vichenza na malimao Mechi zake, huwa hatari Ni chenga na mabao Kazini sionekani, yupo wapi huyu Simuni sipatikani, yupo wapi huyu Baba kaniulizia, yupo wapi huyu Mama aishi kulia, yupo wapi huyu mimi Nimezama katika kina kirefu Cha bahari ya mapenzi Msinitafute, nimezama (Msihangaike katika kina kirefu) Nipo salama, (Cha bahari ya mapenzi) salama, salama mimi Nipo salama mimi, Nipo salama mimi Msinitafute, Nipo salama mimi
Writer(s): Mbwana Yusuph Kilungi Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out