Crediti
PERFORMING ARTISTS
MwanaFA
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Hamis Mwinjuma
Songwriter
Testi
[Verse 1]
Naota ndoto hazina rangi, naamka nazipaka
Watoto wa kiswazi huwezi ukatuwekea mipaka
Mungu ndio ametaka, jongoo kawa nyoka
[Verse 2]
Hakuna kiunzi hatuwezi ruka
Tushasukuma sana milango iliyoandika vuta
Niamini na inafunguka
Mbwa mkali usikatize,wahuni tunapita
[Verse 3]
Tunayavuka kwa kamba madaraja yaliyovunjika
Mungu wetu halali,wala haendi likizo
Hatuachi kumuomba na anafuta matatizo
Yakija tena naomba tena na Mungu anayafuta tena
[Verse 4]
Mioyo yetu ipo safi,safi ile kinoma
Kifo kiniue au maumivu yanikomaze
Yote sawa ila ujinga usinipumbaze
Kila kiumbe ana njaa yake,moyo na tamaa zake
Mbwa mpumbavu ndio anaweza bwekea ndege
[Verse 5]
Waitee wamuone Gwiji wajigambe
Waite, waite waje wamuone Gwiji wajigambe
Waitee wamuone Gwiji wajigambe
Waite, waite waje wamuone Gwiji wajigambe
[Verse 6]
Mi ni hustler babe that's what I do, I hustle
Shida hazikwepeki zipo kukupima muscle
Zikutoe macho, zikutoe jasho
Zikupe akili na zikuandae kwa kesho
[Verse 7]
Jikaze mwana usichukuliwe mateka
Ka unaachana na dunia we ndio uandike talaka
Ukiomba mafanikio fahamu yanakuja na wivu
Havitengani havikai mbali, kidevu na ndevu
[Verse 8]
Dunia haitasimama ukigoma kutembea nayo
Sio magumu ka ku'click link kwa bio
Kakamaa nakupa moyo umegusa tu button siyo
Kuwa mpambanaji kama binamu yangu Suyo
Huu sio mziki wa mafala,ni mziki wa mataita
Unakuweka kitako na chaki unakufundisha
Una'feel the passion,zaidi ya Telemundo
Mapanchi mengi hata Touch akizima mdundo, bye-bye
[Chorus]
Waitee wamuone Gwiji wajigambe
Waite, waite waje wamuone Gwiji wajigambe
Waitee wamuone Gwiji wajigambe
Waite, waite waje wamuone Gwiji wajigambe
Written by: Hamis Mwinjuma

