Letra

Nimekuwa bubu nimepigwa na butwaa Mdomo mzito kinywa kama ndondocha Macho yana magugu sioni mbele najikwaa Yani ujanja sina nimezorota Naona! Joto si joto baridi si baridi Mwili wa nchoma choma Naona! Kichwa kinawaka moto Moyo unakwenda speed Yani homa si homa eeeeh! Vipimo nimemaliza kwa manguri daktari Waganga matabibu eeeh eh! Kumbe najilimbikiza maumivu makali Naongeza maswahibu oooh! Ooh! Nimezunguka kote buza na yombo dovya Sijaaambulia chochote zaidi ya kuchovya chovya Rudi tuishi sote ujinga tu uliniponza Jaribu kusahau yote mtima uje kuupoza Baby fanya! Turudiane turudiane tena Turudiane tuwe kama zamani Turudiane fanya turudiane turudiane Turudiane tena unirudie baby Turudiane tuwe kama zamani Turudiane Yalopita yamepita si ndwele Rudi tugange yajayo we nimekuzoea Tufanye yamekwisha uje tujenge ya mbele Yale tuachane nayo mwenzako najidodea Rudi tufunike kombe mwanaharamu apite Tusijali tutaonekanaje kwa ndugu jamaa Nimekubali kwako kibonde acha tu nidhalilike Sina habari ata wakisemaje nnachotaka furaha Yale matusi kejeli, vijembe, mafumbo kutupiana Yote tufanye yaishe eeeeh eeh! Najua twapendana kweli sasa ya nini tunazozana Rudi penzi tudumishee ooooh oooh! Nimezunguka kote buza na yombo dovya (Nimezunguruka kote) Sijaaambulia chochote zaidi ya kuchovya chovya (Oooh oh, Oooh oh!) Rudi tuishi sote ujinga tu uliniponza Jaribu kusahau yote mtima uje kuupoza Baby fanya! Turudiane turudiane tena Turudiane unirudie Tuwe kama zamani Iyeeeh! Fanya turudiane turudiane Turudiane tena unirudie baby Turudiane tuwe kama zamani Turudiane
Writer(s): Lava Lava Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out