Letra

Uniongoze bado nakuhitaji uniongoze yesu kiongozi mwema moyo wangu nakuhitaji niongoze nivuke salama Mungu wangu uniongoze.Ulisema naposhindwa nikuite hivi leo nakuita nisikie usiende mbali nami usiniache pekee yangu Mungu wangu uniongoze Dunia hii ina mabo mengi sana baba Sasa dhambi imetawala dunia Waliookoka wengine wanarudi nyuma Me napenda nikupendeze Mungu upendezwe nami niyashike maagizo yako unifurahie Neno lako Yesu likae ndani yangu Kuna wengine wachanganya Mungu na dunia Na wengine wanalibadili neno lako Yesu ukisema na wao pia wanasema Me nataka nikusikie Yesu ukisema nami Maana wewe ndio wa thamani maishani mwangu Nguvu zako yesu zikae ndani yangu Ni kweli bwana nimekutana na vita kali Lakini yesu umepigana badala yangu Wewe umekuwa ni mwamba wa wokovu wangu Mbele yangu sijui kuna nini unipiganie Usipokuwa nami sitaweza kitu unishikilie Natamani sana nione uso wako Jemedari wangu
Writer(s): Upendo Nkone Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out