Lyrics

Mmmmm ye ameniona huyu Yesu ee Hallelujah mmmmm. Mimi nilikuwa kipofu muda wa siku nyingi Sikupata msaada kwa mwanadamu yeyote Yesu alipokuja kapaka udongo machoni mwangu Sasa nimeona acha nishuhudie makuu yake hallelujah Ooooo Yesu ameniona Ooooo Yesu ameniona Mimi nilitokwa na damu miaka kumi na miwili Waganga na madaktari hawakuweza kuniponya Nilipomuona Yesu nikagusa pindo la nguo yake Damu ikakauka sasa mimi nimepona hallelujah Ooooo Yesu ameniona Ooooo Yesu ameniona ×2 Nilitoza kodi miaka mingi iliyopita Niliwaibia watu wengi waliteseka kwa ajili yangu Nikapanda juu ya mti Bwana Yesu akaniona akanisamehe nikalipa madeni yote hallelujah Ooooo Yesu ameniona Ooooo Yesu ameniona ×2 Ameeeeeeniona ameniona Yesu wangu Ninapo-omba mimi ninapo-lia mimi Nipitapo chini ya bonde la uvuli wa mauti Yesu wangu ameniona Hallelujah
Writer(s): Angela Chibalonza Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out