Lyrics
Yote hayo yanakuhusu wewe?
Eh, mchungaji, mchungaji, nimekuja, kuja nikuelezee habari za huyu mama
Huyu mama unavyomwona alikuwa na ngombe, alikuwa na kuku, kila aina ya mfugo
Vimekufa, anasema, "Jaribu", huyu katenda dhambi huyu
Umetenda dhambi
Ni majaribu ambao nayapitia
Jaribio namna gani?
Kwanzia leo hiii sitaki kukona tena hapa kanisani
Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambi
Ila ni kikombe tu ambacho ni lazima akinywe
Jaribu kwa mtu si kwamba kakosa kwa Mungu
Ila ni wakati tu ambao ni lazima apitie
Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambi
Ila ni kikombe tu ambacho ni lazima akinywe
Jaribu kwa mtu si kwamba kakosa kwa Mungu
Ila ni wakati tu ambao ni lazima apitie
Usimwone mtu anapita kwenye jaribu
Anavumilia kwa sababu ni wakati wake
Maumivu aliyo nayo hawezi mpa mtu
Ananyamaza kwa sababu ni kikombe chake
Hakuna aliyewahi omba kwa Mungu apitie
Yale anayoyapitia
Hakuna aliyesema na Mungu yampate
Yale, yale yanayompata
Jaribu lingeondolewa kwa kuomba sana
Wote tungeomba tusipite kwenye jaribu
Jaribu lingekwepeka kwa kufunga sana
Ndungu yangu, wengi tungefunga tusipite kwenye jaribu
Jaribu lingeondolewa kwa kuomba sana
Wengi tungeomba tusipite kwenye jaribu
Jaribu lingekwepeka kwa kuomba sana
Ndungu yangu, wengi tungefunga tusipite kwenye jaribu
Mtu mwenye jaribu hajaomba kwa Mungu
Ni wakati tu anapitia
Mtu mwenye pito hajaomba kwa Mungu
Ni wakati tu, ni wakati anapitia, heh, heh
Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambi
Ila ni kikombe tu ambacho ni lazima akinywe
Jaribu kwa mtu si kwamba kakosa kwa Mungu
Ila ni wakati tu ambao ni lazima apitie
Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambi
Ila ni kikombe tu ambacho ni lazima akinywe
Jaribu kwa mtu si kwamba kakosa kwa Mungu
Ila ni wakati tu ambao ni lazima apitie
Kulikuwa na Ayubu aliyemcha Mungu
Mungu mwenyewe alijivunia Ayubu
Ayubu hakujua kwamba ipo siku moja
Itafika atapita kwenye majaribu
Ayubu hakuwaza kwamba ipo siku moja
Itafika atapita kwenye jaribu
Siku moja Mungu akakutana na shetani
Akasema, "Shetani wewe, umetoka wapi?"
Shetani akajibu, "Nimetoka duniani nikizunguka zunguka huku na kule"
Mungu akasema, "Umemwona mtu wangu?
Hapana mtu mwema kama Ayubu"
Shetani akasema, "Ni kwa sababu umezingira pande zote huyo
Jaribu kutoa kila kitu uone kama Ayubu hatakutenda dhambi"
Ayubu akaanza kupitishwa kwenye taabu
Yote kwa sababu Mungu alijivunia Ayubu
Ayubu akaanza kupitishwa kwenye mateso
Yote ni kwa sababu Mungu alijivunia Ayubu
Ayubu hakujua kwamba Mungu wa Mbinguni anajivunia yeye
Alipitia mengi, alisongwa na mengi
Yote ni kwa sababu Mungu alijivunia Ayubu
Alisongwa na mengi, alipitia Mengi
Ayubu akasema, "Pamoja na yote nitaishi"
Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambi
Ila ni kikombe tu ambacho ni lazima akinywe
Jaribu kwa mtu si kwamba kakosa kwa Mungu
Ila ni wakati tu ambao ni lazima apitie
Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambi
Ila ni kikombe tu ambacho ni lazima akinywe
Jaribu kwa mtu si kwamba kakosa kwa Mungu
Ila ni wakati tu ambao ni lazima apitie
Ndipo nimejua kumbe yote yanipatayo mimi ni kwa muda
Sijatenda dhambi, hujatenda dhambi ni wakati tu lazima tupitie
Msimwone mtu analia sasa ni Mungu anajivunia huyo
Kumbe mengi yanatukuta sisi hatujui lakini Mungu anajivunia sisi
Anajua mwanzo, anajua mwisho, ni Baba anajivunia sisi
Unapitia mengi, unasongwa na mengi
Kumbe ni Mungu anajivunia wewe
Tulia kwa Mungu, tulia kwa Baba ili mwenyewe ajitukuze kwako
Kweli tunachoka, kweli tunashindwa, aki ni Mungu anajivunia sisi
Hatuwezi kuwa washindi, hatuwezi kung'aa sana, lazima Mungu ajivunie
Hatuwezi kuendelea, hatuwezi kuvuka ng'ambo, ni lazima tupitie haya
Jaribu lako ni wakati tu Mungu anajivunia
Jaribu lako ni wakati tu, ni wakati unapitia
Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambi (kwa mtu anapitishwa kwa muda)
Ila ni kikombe tu ambacho ni lazima akinywe (ata vuka tuu, asha apitishwe leo)
Jaribu kwa mtu si kwamba kakosa kwa Mungu (kwa muda tuu, ni wakati tuu)
Ila ni wakati tu ambao ni lazima apitie (asha buga, wengi wameliya)
Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambi (wengi wameshoka, lakini ni kwa muda)
Ila ni kikombe tu ambacho ni lazima akinywe (ni kikombe tu)
Jaribu kwa mtu si kwamba kakosa kwa Mungu (aja kosa kwa Mungu, ni wakati tu)
Ila ni wakati tu ambao ni lazima apitie (ni wakati wake)
Written by: Martha Mwaipaja