Credits
PERFORMING ARTISTS
Rostam
Performer
Roma & Stamina
Background Vocals
COMPOSITION & LYRICS
Ibrahim Musa
Songwriter
Boniface Kabogo
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Ibrahim Musa
Assistant Producer
Lyrics
Naona mkandaa unakatika uko kimya sana mkato au kundi limevunjika
Na utanyooka raundi hii na hivi huwezi bila mimi?
Najikuta Jay Z oya unarudi lini?
Kaka, huku wamefunga mipaka, ila tiketi nilikata nirudi kabla pasaka
Rudi ugeuze kisu sio mwana kulitafuta mwana kulipata, raundi hii sio ununio daraja la
Basi kumekucha, ni saa ngapi huko nipe takwimu
Nimeamka nishaweka bundle namwongoja Ummi Mwalimu
Anapambana yule dada
Tanga nimewavulia kofia, wametosa sanitizer za iliki yaani ukipata unalipia
Corona nishai, yaani bongo kila mtu daktari, maasai kachemsha majani ya mpapai kanywa na sukari
Buza hadi maski wanafua, sijui nani kawafundisha
Huku kuna dada kajifukiza, mashetani akayapandisha
Tueke siasa kando, unajuwa uchumi unashuka?
Sio bongo tu hadi ng'ambo, watu wamefunga maduka
Hapa nawaza pesa ya pango, benki waliokopa wanajuta, tukisema tukae ndani, na hii njaa si tutakufa?
Hali inatisha na umaskini, tunaoumia ni sisi
Yaani bora ufe kwa ukimwi, angalau utaandika urithi
Kwa hiyo hamna bata, sio kidimbwi sio tipsi
Kaka madanga wamekata, so hazitimbi hizo pisi
Bwana wa mabwana, Mungu wa miungu, Alpha na Omega, nani kama wewe?
Bwana wa mabwana, Mungu wa miungu, Alpha na Omega, nani kama wewe?
Hivi unakaa jimbo gani au Marekani ya vijijini, unajikinga vipi maana vifo vingi hadi siamini
Au umesharudi, uko zako rohoro nini?
We, bana ebu niache mi nimeze Chloroquine
Umenikumbusha, kwani Chloroquine ni dawa?
Bado inafanyiwa uchunguzi ila haijathibitishwa
Ingawa ukinywa haitatarisha ndio maana bado wanaigawa, mi nakunywa maana nilishika uso kabla ya kunawa
Eti unaweza ukawa nayo na usionyeshe dalili?
Ewaa, uko sahihi na kingine kuhusu hili ni kwamba mgonjwa wa Corona unaweza usimtambue kwa macho
So mtu yeyote unamwona mpe mita mbili toka kwako
Na hiko kifanslika ndio kinini baba Willy?
Ni ventilator ni mashine ka mapafu ya nje ya mwili
Sijaelewa, embu nieleweshe kuhusu hili, nasikia vinauzwa ghali, basi vile vingi mwimbili
Okay, kirusi cha korona kinashambulia mapafu
Ndipo zinaanza homa, mafua ya kifua, halafu unashindwa kupumua na mwili unahitaji dafu, ventilator huingiza hewa na kuitoa iliyo chafu
Tuepuke mikusanyiko ikibidi tukae ndani
Tumeambiwa tujifukize hivi ni dawa unadhani?
Ngoja kwanza, hivi fumigation
Mmm mmm, baba ile inaua mende, acha utani
Bwana wa mabwana, Mungu wa miungu, Alpha na Omega, nani kama wewe?
Bwana wa mabwana, Mungu wa miungu, Alpha na Omega, nani kama wewe?
Maisha ya upweke yanasumbuwa, ila siku zinapita
Yule mkewe itunze pete mtayamaliza na uhakika kaka
Kila hatua dua, haina haja ya kusikitika
Ila navyokujua, kweli hujazini miezi sita
Kiukweli mi mwaminifu, ingawa jogoo anawika
Mama Ivanny mabalifu hakuchiti una uhakika? Kuna mchezaji wa Yanga, namuona anapita-pita
Ntamkata-kata mapanga, yaani namuua na namzika
Oyah wape nyumbani, basi pesa ya matumizi
Kaka nitoe wapi, na show hakuna sikuhizi
Hali imekuwa ngumu hakuna pesa kila corner, kila mtu unayemdai naye anasingizia Corona
Mbona sasa wanafunga shule na vyuo halafu bar hawafungi
Mzazi atamlindaje mtoto na akirudi yupo tungi
Polisi India wanapiga watu wakisongamana, wao wabarakoa wanajua hadi fender wamebanana
Sasa wanatukusanya kutuambia tusikusanyike, ila wauguzi wanajitoa sana, duh, Mungu awalipe
Wapinzani mnatangaza vifo walopona hamwatangazi
Wanasema mungeeka takwimu za wazi ingekuwa kizazi
Kwa hiyo lockdown hakuna halafu umeona texti niliotuma?
Ipi? kwenye group, mbona inbox hakuna?
Nasikia, nini? Kwa Yuzee Kambochi
Maana huko uliko usiongee sana inatosha
Hadi papai lina Corona! duh, kaka tuchati
Na mbuzi vipi? Ee eh kaka tuchati
Mwili umekufaa ganzi, kaka tuchati
Poa mwanangu tundelee kujifukiza
Written by: Boniface Kabogo, Ibrahim Musa