Lyrics

Mteule Uwe Macho – Rose Muhando Ooh ye dunia sasa ni mashakani Kumbe dhambi imekuwa kitu cha kushangiliwa Kwa gharama kubwa imejengewa ngome za kifahari Ooh ye dunia sasa ni mashakani Kumbe dhambi imekuwa kitu cha kushangiliwa Kwa gharama makubwa imejengewa ngome za kifahari Mabomu ya kujitoa muhanga ni jambo la hatari Umwagaji damu isiyo hatia ni jambo la kutisha Yaliyonenwa na nabii Danieli sasa yanatimia Ni nani atasimama, mbele ya hasira ya Bwana Atulize ghadhabu yake isiipate dunia Ni nani atasimama, mbele ya hasira ya Bwana Atulize ghadhabu yake isiipate dunia Eeeh, lelelelelelele Mteule uwe maaaacho Ni siku za mwisho nasema Mteule uwe macho, hizi ni siku za mwisho Kwani yale yaliyotabiriwa sasa yanatimia Tusimame imara tujifungeni mikanda Kwa silaha za haki kifuani, na tusonge mbele Mpingeni shetani, mnyang'anye mamlaka Tupilia mbali tamaa ya dhambi, weka pembeni Uwe macho, hizi ni siku za mwisho Kwani yale yaliyotabiriwa sasa yanatimia Tusimame imara tujifungeni mikanda Kwa silaha za haki kifuani, na tusonge mbele Mpingeni shetani, mnyang'anye mamlaka Tupilia mbali tamaa ya dhambi, weka pembeni Kutangatanga kwako wewe, mbona kwa kuchelewesha Nachelewa kusema nawe, utafuna ulichopanda Shika sana ulicho nacho, Yesu yu karibu kuja Mwenye sikio asikie, roho asema na kanisa Eeeh, lelelelelelele Ah yayayayaya (Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi) Muongo endelea kutenda dhambi, dunia ikujuee (Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi) Mumbea endelea kusema umbea, vunja nyumba za watu (Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi) Mchawi endelea kuroga sana, mchana peupee (Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi) Wachungaji tuelezeni, mwatupeleka wapi jamani Mbona Asikofu mwanamume, ameoa mume mwenzie Andiko hili latoka wapi, tena kwenye Bibilia gani Watoto wetu wa kiume, tuwafiche wapi jamani Wamama nao bila aibu, wazini na vijana wadogo Sasa tutapataje kupona, ukimwi utatumaliza Eeeh, lelelelelelele Ah yayayayaya (Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi) Kahaba endelea kufanya ukahaba, mpaka kwenye internet (Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi) Malaya endelea kufanya umalaya, utakwenda na ngoma (Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi) Washerati endelea kufanya dhambi, Yesu yuaja (Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi) Lokole endelea kujitakaza, Yesu yuaja (Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi) Shoga endelea kufanya ushoga, mpaka kwenye mtandao (Eh, mwenye dhambi wewe, endelea kutenda dhambi) Eeeh, lelelelele Jamani nasema Mteule uwe macho, hizi ni siku za mwisho Kwani yale yaliyotabiriwa sasa, yanatimia Tusimame imara, tujifungeni mikanda Kwa silaha za haki kifuani, na tusonge mbele Mpingeni shetani, mnyang'anye mamlaka Tupilia mbali tamaa ya dhambi, weka pembeni Uwe macho Oh, yeyeye, yeyeye Oh yeyeyeye Uh yeyeyeyeye
Writer(s): Maureen Nkirote Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out