Credits

PERFORMING ARTISTS
Ben Pol
Ben Pol
Background Vocals
COMPOSITION & LYRICS
Benard Paul
Benard Paul
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Ben Pol
Ben Pol
Producer

Lyrics

First time nilipenda nikajiona nimefika
Nikajua sitotendwa machozi yasinge nitoka
Nikajihadaa nikajawa na furaha
Mwishowe kushituka nimezimia balaa
Kaniacha ingawa alijua kabisa
Pasi na penzi lake mimi sina maisha
Akaniumiza nikadhoofika
Nikajifariji na siku zikapita
Nakumbuka nikasema sitokuja penda tena
Baada ya miaka kupita nikajiona nishapona
Nikayasahau maumivu ya nyuma
Na nikajikuta nimependa tena
Sikuamini kabisa kilichotokea tena
Machozi ya mapenzi kunibubujika tena
Ikanifanya nasema sitaki kuumizwa tena tena
Wengine mbona wanajali upendo
Wengine mbona mwaumiza tu
Nyinyi nimewapatia langu pendo
Wakalivunja na kuacha vidonda
Wengine mbona wanajali upendo
Wengine mbona waumiza tu
Nyinyi nimewapatia langu pendo
Wakalivunja na kuacha vidonda
Kila ajaye hunitumia na kwenda zake
Hathamini uhitaji wa moyo wangu kwake
Nami nimekua kulia na kupona
Kila siku bora kutopenda tena
Najua ni vigumu kuishi bila penzi
Lakini bora hivo kuliko machozi
Sijui labda mi nina mkosi gani?
Wengine mbona wafurahi penzini?
Tamu ya mapenzi siijui mimi
Chungu na mimi maumivu moyoni
Tamu ya mapenzi siijui mimi eeh
Tamu ya mapenzi siijui mimi
Chungu na mimi maumivu moyoni hey (ooh)
Wengine mbona wanajali upendo
Wengine mbona mwaumiza tu
Nyinyi nimewapatia langu pendo
Wakalivunja na kuacha vidonda
Wengine mbona wanajali upendo
Wengine mbona mwaumiza tu
Nyinyi nimewapatia langu pendo
Wakalivunja na kuacha vidonda
Written by: Benard Mnyanganga, Benard Paul
instagramSharePathic_arrow_out

Loading...