album cover
Ukuta
album cover
Ukuta was released on March 27, 2026 by AICT DODOMA CHOIR as a part of the album Ukuta - EP
March 27, 2026
LabelAICT DODOMA CHOIR
BPM176
Melodicness
Acousticness
Valence
Danceability
Energy

Lyrics

Ukuta huo uko mbele yako
Yeriko hiyo iko mbele yako
Je utaikabili au utaogopa
Amua kutii maagizo ya Bwana, utamuona
Chukua hatua kumsikia Bwana, anavyosema
Na uzunguke zunguke, uzunguke zunguke, uzunguke zunguke
utaona matokeo yake
Israeli kuuingia yeriko, iliwapasa kuuzunguka ukuta
Kwa maagizo waliyopewa na Mungu,
Kwa siku sita walizunguka ukuta, bila ya mafanikio yoyote
Siku ya saba nguvu za Mungu zilishuka,
Ukabomoka ukuta, wakauteka yeriko
Hata na wewe umekutana na jaribu,
Jaribu lako limegeuka ukuta, usiogope zunguka
Zunguka kwa maombi
Zunguka kwa imani
Zunguka wee ukimwamini Bwana
Zunguka wee utashinda
Amua kutii maagizo ya Bwana, utamuona
Chukua hatua kumsikia Bwana, anavyosema
Na uzunguke zunguke, uzunguke zunguke, uzunguke zunguke
utaona matokeo yake
Mungu si dhalimu, ameutia yeriko mikononi mwako
Mungu si dhalimu, anachotaka ni wewe utii maagizo yake
Maagizo yake ni wewe ulijue neno lake
Maagizo yake ni wewe umtafute kwa bidii
Maagizo yake ni wewe uongeze imani yako
Maagizo yake ni wewe, umsikilize
Na uzunguke zunguke, uzunguke zunguke, zunguke wee
Utaona matokeo yake
Na uzunguke zunguke, uzunguke zunguke, uzunguke zunguke
utaona matokeo yake
Written by: Samwel Limbu
instagramSharePathic_arrow_out􀆄 copy􀐅􀋲

Loading...