Şarkı sözleri

Mtu mmoja alistaajabu sana, niliposema nitamshukuru Mungu Baada ya matatizo mengi kunipata akili yangu ikampa wasiwasi Kwa kweli nami, ilinigharimu, kujijulisha inipasavyo Ila baada ya muda nikaona yapo mengi ya kunifanya nimshukuru Mungu Yako mengi, hayajakwisha yatubidhishayo tumshukuru Mungu wetu Japo twapita majaribu mengi bado, yapo mengi ya kushukuriwa (Jiunge), he, ee, jiunge nasi, tulisisitize jambo hili la muhimu Yale yote tujiulizayo mioyoni majibu anayo Mungu wetu Ambassadors of Christ tuashukuru lakini kwa wengi hatueleweki Kutokana na mambo ya yaliotupata ivi kushukuru si jambo la busara Lakini ndugu (eh), ukitulia, nakujiuliza ya ajali ile Tungeweza kuangamia wote kwa pamoja asiwepo hata mmoja wa kusimulia Yako mengi, hayajakwisha yatubidhishayo tumshukuru Mungu wetu Japo twapita majaribu mengi bado, yapo mengi ya kushukuriwa (Shukuru), he, ee, jiunge nasi, tulisisitize jambo hili la muhimu Yale yote tujiulizayo mioyoni majibu anayo Mungu wetu Majaribu kama haya yalikuweko hata kwenye siku za mababu zetu Ila kwa yote walikuwepo mashujaa walioweza kuitetea imani yao Tuwake Mungu (eh), wakati wote, kwa yote hatujitegemei Tukiwa hai tukiwa mauti tuwake tujualo ni moja kushukuru Yako mengi, hayajakwisha yatubidhishayo tumshukuru Mungu wetu Japo twapita majaribu mengi bado, yapo mengi ya kushukuriwa (Jiunge), he, ee, jiunge nasi, tulisisitize jambo hili la muhimu Yale yote tujiulizayo mioyoni majibu anayo Mungu wetu He ee jiunge nasi, tulisisitize jambo hili la muhimu Yale yote tujiulizayo mioyoni majibu anayo Mungu wetu
Writer(s): Ambassadors Of Christ Choir Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out