歌词
Chocheeni kuni mbichi, moto ukoleee, ugali uive
Mnacho taka kitokee, alikeni mamluki wakija wangojee
Mikeka wawekee, wanachotaka kitokee
Chochea, chochea, chochea, chochea
Chochea, chochea, chochea, oh, chochea
Chochea, chochea, chochea, chochea
Chochea, chochea, chochea
Watanzania, mwenda kwao sikuzote haogopi giza
Acheni nirudi nyumbani, safari imenishinda
Nauli zenu ntarudisha
Mtu anatapika nyongo yake, anailamba tena anaangaliwa
Ni sawa na tawi kavu linapoanguka, watu wakapiga kelele, aya!
Katika misimu minne kwa mwaka, tuongeze musimu mwingine wa tano wakujishtusha
Raha ya jamvi sikuzote ni viraka viraka
Na dungu linamficha mlinzi wa ndege wakati wa mvua tu
Eti, oh, imenyesha juzi tu
Maji sio mengi, nisubirini kule
Ilishindikana vipi kuyapima maji kwa mti, ndio mkawaambia watu wavuke?
Mjomba, binadamu ni kama ganda la kitabu, paka umfungue maandishi ndio uweze kumuelewa
Eti, lililotokea mbali tufanye limepita, na haliwezi kumdhuru mwingine
Kweli? Inayotaka kunyesha, hua haisubiri mawingu
Mimi sidhani, kama kujiponya kwa mambo mzito tubahitaji cheti kilichigongwa mhuri wa moto
Au mtaalamu wa magonjwa ya akili, zaidi yakutumia neno sahau
Unawaulizaje watu magongo ya nini wakati umesema kuna nyoka?
Mjomba, wewe si uliwapaka wanja?
Ngoja wao wakupake pilipili, alafu kwenye kimbolela iwe zamu yako kuzinga
Chocheeni kuni mbichi, moto ukoleee, ugali uive
Mnacho taka kitokee, alikeni mamluki wakija wangojee
Mikeka wawekee, wanachotaka kitokee
Chochea, chochea, chochea, chochea
Chochea, chochea, chochea, oh chochea
Chochea, chochea, chochea, chochea
Chochea, chochea, chochea
Mngekuwa mnajua anachokula nyuki, msingethubutu kusema asali ni tamu
Niwashukuru, kwa kufikiri mjini mimi nilifaha niende
Halikuwa wazo baya kwa wakati ule
Maana mlionyesha ukomavu kutoka kwenye shingo kwenda chini na sio juu
Mbona hamkumfikiria aliyekuwa ndani, kafungiwa kwa nje?
Usingizi hapati anawaza jinsi ya kutoka
Nikisema uwezo wa watu kufikiri na mahitaji unatofautiana
Mtaanza kusema nina dharau na matusi
Lakini kumbukeni ulimi unauma kuliko meno
Mnawezaje kumfikiria aliyekuwa ndani, kajifungia mwenyewe
Funguo anazo mwenyewe kalala fo fo fo
Asijue hata idadi ya misumari iliyoshikilia mlango wake
Kulipamba jeneza, hakumfanyi aliyekufa kufufuka nyinyi
Kama kusema nimeshasema sana, mwishowe nitakuwa kama mwanasiasa
Hawajitokezi mpaka kuwe na maafa
Natoa katoni ishirini za sabuni ya unga, aliyekwambia wale wachafu nani?
Kasafisheni kwanza nyoyo zenu ndio mrudi kwa wananchi
Ndugu zangu, tawi kavu, kuanguka wala sio ajabu
Wakati wao wanatenganisha mavi ya panya kwenye unga
Nyinyi chocheeni kuni zilizoloa, maji yapate moto ugali usongwe
Wakiwauliza, waambieni huu ni utani
Hapa kwetu tuna makabila mia moja na ishirini, tunataniana
Waliopo hatuwataki, wanaotaka hatuwaamini
Maneno siku zote yanauma na yanachefua ukijua maana yake
Kwa mfano neno la kitoto, mtoto kumwambia mtoto tunasema watoto wanacheza
Neno la kitoto,mtoto kumwambia mkubwa tunasema mtoto anakua
Mtoto akisema babaa, ile ndege yangu
Baba hata kama huna baiskeli, unamwambia ikitua nitakuletea, ndio utaratibu
Lakini maneno ya kitoto, mtu mzima kumwambia mtu mzima mwenzie, kuna walakini
Mimi safari imenishinda, na sitaki tena kuulizwa kwanini
Chocheeni kuni mbichi, moto ukoleee, ugali uive
Mnacho taka kitokee, alikeni mamluki wakija wangojee
Mikeka wawekee, wanachotaka kitokee
Chochea, chochea, chochea, chochea
Chochea, chochea, chochea, oh chochea
Chochea, chochea, chochea, chochea
Chochea, chochea, oh, oh
Written by: Mrisho Mpoto