Lyrics

Mmmh mmmh Mama ananiambia Nasibu Mimi ni mtu mzima na we ndo nakutegemea Yanayotokea jaribu kupiga kimya Usidiriki hata kuongea Mara nasikia vya aibu Konda Gwajima eti ugomvi umekolea Kuchunguza karibu Ni binti mmoja kwa mitandao anachochea Najariibu kunyamaza, ila moyo utaki Unaniambia eti Simba japo nguruma uisemee haki Oooh najaribu kunyamaza hata Laizer hataki ooh Anasema walau nena kidogo Na mashabiki Dangote Wananiambia mbona husemi chochote Aah si uko nao siku zote, ama ulezi unafanya uogope Aah na media pande zote wanalalama kiongozi Atoke Nchi inaingia matope Niende wapi na mi mtoto wa wote (Yani Lawaama) Acha nikae kimya (nisiongee) (Kimya) ooh ninyamaze mimi Nikae kimya, nisiseme (kimya) Mama kanambia (wacha nikae kimya) Oooh nifunge mdomo (kimya) Mie bado mdogo sana (kimya), nisiseme (kimya) Mmmh ni mengi majaribu najitahidi epuka yasijeni-cost Japo mengine swadakta mengine hayana maana Rafiki kipenzi wakaribu ata nyimbo yake sikueza ipost Ila alivokamatwa iliniumiza sana Mitandao kila kona Uongo na ukweli unashonwa Kila nyumba inanongona Aaah Ooh Tanzania Mara kimbembe Dodoma Bunge wapinzani wameg'oma Juzi akapotea na Roma Ooooooh Tanzania ooooh Najariiibu kunyamaza Makame hataki oooh eh Ananiambia walau nena kidogo Nyumbani nafungua geti Niende kwa mangi nunua spaghetti eeh Napewa za chini ya kapeti Kuna redio imevamiwa eti Eeh napita kwenye magazeti Nakuta rundo la watu wameketi eeh Badala ya kutafuta senti Wanabishana tu mambo ya vyeti Wacha nikae kimya (oh nisiongee) (Kimya) ninyamaze kabisa (nikae kimya) Ulimi koma (kimya) Usijekuniponza (wacha nikae kimya) Nifunge bakuli langu (kimya) Nikojoe nikalale (nikae kimya) Me bado mudogo sana (kimya) Mama kanambia Ooooh najiuliza (wapi) Najiuliiza (wapi) Tunakwenda wapi (wapi) Kila siku maneno (wapi) Ah tuacheni jamani (wapi) Me na we ni taifa moja (wapi) Kambarage baba mmoja (wapi) Sa tofauti za nini tushikamane (wapi) Tukaijenge Tanzania
Writer(s): Naseeb Abdul Juma Issack Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out