Lyrics

Oooh aaah Aaah... Achana na hao manyambafu, wasikupande kichwani Midomo yao michafu, isikunyime amani We nipende kama sarafu, unifiche kwapani Na unigande siafu, hata tukiwa njiani Hawapendi kuona penzi linafika mbali Udi wanachoma, usiku wala hawalali Wanakesha kwa sangoma, penzi walitie misumari Wasikupee homa, mambo yatakuwa ng'aring'ari Eeeh Naomba zifikisheni habari Kwa Rikadomomo Kurukushani za Mondi na Zari Zimenipa somo (Hatuachani, hatuachani) (Hatuachani), mimi naye darling (Hatuachani), tunalicheza rhumba (Hatuachani), mimi naye darling (Hatuachani), tunalisakata rhumba (Hatuachani), mimi naye darling (Hatuachani), tunalicheza rhumba (Hatuachani), mimi naye darling (Hatuachani), tunalisakata rhumba Wala usijaribu Kuwapa nafasi wafukunyuku Watakutia aibu Zao kubwabwaja kama kasuku Kujifanya wataratibu Hawana lolote mazumbukuku Wana maswahibu, waongo Hata mwezi mtukufu Tusile tembele Kisamvu kwa nyama Wataona gere Na kutusakama Vibwabwa jengere Na vikuku vya ngama Watapiga ndele Vipate kutukwama Wao wapae na ungo sisi hatujali Yatawakereketa wavimbe matumbo Hatuna habari eeh Wao wapae na ungo sisi hatujali Yatawakereketa wavimbe matumbo Hatuna habari Eeeh Naomba zifikisheni habari Kwa Rikadomomo Kurukushani za Mondi na Zari Zimenipa somo (Hatuachani, hatuachani) (Hatuachani), mimi naye darling (Hatuachani), tunalicheza rhumba (Hatuachani), mimi naye darling (Hatuachani), tunalisakata rhumba (Hatuachani), mimi naye darling (Hatuachani), tunalicheza rhumba (Hatuachani), mimi naye darling (Hatuachani), tunalisakata rhumba Agah Rhumba mama rhumba Tulicheze rhumba Rhumba mama rhumba Tulicheze rhumba Rhumba mama rhumba Tulisakate rhumba Rhumba mama rhumba Tulicheze rhumba Agah Tulicheze (rhumba) Tulisakate (rhumba) Tulicheze (rhumba) Tulisakate (rhumba) Apo Apo
Writer(s): Lava Lava Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out