Lyrics

Hapa nilipo mimi nipo kitandani Starehe zimeniweka matatani Kupona tena mimi haiwezekani Masela wangu ndugu zangu buriani Kwaherini, kwaherini, kwaherini Sua side Scott Jenta kwaherini Bongo Record na Majani kwaherini Hamtoniona tena duniani Sasa najuta, mwenzenu yamenikuta Ibilisi amefanikiwa kunivuta Sasa sijui wa kumlaumu nani Kati ya nafsi yangu ama shetani Kwaherini, kwaherini, kwaherini Makongo na Jiteute, kwaherini Mohaa na Azania, kwaherini Aan haa, haaa, haaa Saa saba juu ya alama saa nikiitazama Nimeshaachana na Jacki sasa namfata Salama Saa kumi na mbili n'na appointment mademu wawili Achana na Lily ambae tutakutana saa mbili Jenny wa Mikocheni ambae sasa hayupo duniani Aliyekuwa akinisubiria pale Vatcan Kijiweni Amina na Semeni tunakutana kwa Macheni Na kila siku nawabadilisha tena kwa foleni Huo ndio uliokuwa mwenendo wa maisha yangu Mimi viwanja kujivinjari na machangu, oh ooh Niliona fahari-ii, yeah Starehe mi nilizifanyia papara Nilibadili mademu kama vidaladala Nikienda nimepanda hili, nikirudi lile Nilitamani starehe zote nizitawale Hata kumkumbuka Mola wangu ilikuwa ndoto Nilitekwa na ulimwengu kumbe naukimbilia moto Katika kubadili wasichana nilikubuhu Nilitembea na watoto wa geti, machangu na masista duu Ubaya kwamba condom sikuitambua Kwa kujua kwamba ladha ya mapenzi itapungua Kumbe nilikuwa ninapotea njia Niliyoshauriwa mimi niliyapuuzia Idadi ya wanawake ikawa lukuki Ikafika kipindi wengine nikawa siwakumbuki Ona, ona, aah Ona sasa yaliyonisibu kwa dada yake Bashiri Nilishamsahau kama tulishakutana kimwili Nilivyomuona, nikamtongoza tena Tena kwa mara ya pili Ona sasa, aah aah Hapa nilipo mimi nipo kitandani Starehe zimeniweka matatani Kupona tena mimi haiwezekani Masela wangu ndugu zangu buriani Kwaherini, kwaherini, kwaherini Afande Sele Morogoro, kwaherini Arusha wanaapollo, kwaherini Hamtoniona tena duniani Sasa najuta, mwenzenu yamenikuta Ibilisi amefanikiwa kunivuta Sasa sijui wa kumlaumu nani Kati ya nafsi yangu ama shetani Kwaherini, kwaherini, kwaherini Discipline Camp na Wakushi, kwaherini Sinza Star na Choka Mbaya, kwaherini Aan haa, haaa, haaa Kijana vipi mbona hujagonga mlango Jipange kwenye foleni mmoja mmoja ndio mpango Ondoa mashaka, tiba bora haihitaji haraka Subiri watibiwe wenzako nawe utafuata Dokta mi nimekuja kufanya hitimisho Naamini hii ndo itakuwa nngwe yangu ya mwisho Dalili zinaonyesha nimeathirika Na nimekuja pima tu nipate uhakika Hebu cheki dokta nilivyokonda Nimebakia mifupa, mwili umetapakaa vidonda Vipele usiseme hii dalili ya umeme Dalili ya umeme, eeh Oh, acha uoga hata malaria hiko namna hii Unaweza ukakonda kwa typhoid au TB Ukinificha unahatarisha maisha Ni bora kubainisha kipi kinakutisha, eeh Homa za mara kwa mara kwangu hazikatiki Kuharisha, kutapika mara sitini na mbili kwa wiki Eh, angalia hata nywele zilivyonyonyoka Mabega yamepanda juu utasema yanachomoka Ninao, ninao (Subiri vipimo) Ninao, ninao (Usikate tamaa) Ninao, ninao Dokta usinipe moyo Ni sawa unampa mfupa autafune kibogoyo Duniani mimi sina umuhimu Kuiaga dunia napaswa inanilazimu Ni bora nijue tu nielekee kuzimu No, no, hayo maamuzi ya ajabu Na ni ulimbukeni kujiua pasipo sababu Maradhi ni kawaida kwa binadamu hilo ufahamu Ni vyema ungetulia upate majibu ya damu Sasa kumbe we unaona mi nasubiri nini? Ni bora tu niwahi kupumzika kaburini Starehe mnazipenda ila mwisho wake mbaya Wengi wameteketea kwa kuendekeza umalaya Vipimo vinaonyesha ni kweli umeathirika I'm very sorry kupoteza nguvu ya taifa Ni vyema kufanya ibada na kumrudia Muumba wako Kula vizuri, fanya mazoezi, pumzisha mwili wako Ukizingatia haya utaishi kwa matumaini By the way, unayo nafasi hebu jiamini Mbona aliyeniumba sasa nishamkosea Hata ardhi na mbingu vyote vinanizomea Malaika wa adhabu kwa hamu wananingojea (Koh, koh) Nikifika huko nani atanipokea, aah, aah Hapa nilipo mimi nipo kitandani Starehe zimeniweka matatani Kupona tena mimi haiwezekani Masela wangu ndugu zangu buriani Kwaherini, kwaherini, kwaherini Wa bara na visiwani, kwaherini TMK, Kino Graid, kwaherini Hamtoniona tena duniani Sasa najuta, mwenzenu yamenikuta Ibilisi amefanikiwa kunivuta Sasa sijui wa kumlaumu nani Kati ya nafsi yangu ama shetani Kwaherini, kwaherini, kwaherini Kikosi Cha Mizinga, kwaherini Migo Migo, Sinza, kwaherini Aan haa, haaa, haaa
Writer(s): Feruzi Mrisho Rehani Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out