Lyrics

Nakushukuru Mungu wangu Kwa mambo yote umetenda Nakushukuru Mungu wangu Kwa yale yote umetenda Tangu sijazaliwa, Tangu sijajijua Wewe ulinitambua Na kuniwazia mema Tangu sijazaliwa, Tangu sijajijua Wewe ulinitambua Na kuniwazia mema Leo niko hapa si kwamba nimetenda mema Bali ni neema zako umenishushia Umenipa uhai umenitia nguvu tena Asante, Asante Nimesafiri salama, nimerudi salama Ni wewe Kwenye maisha yangu nimekuona Wewe Ukinishika mkono na kuniongoza Wewe Hakika ni wema na fadhili zako, wewe Ni kwa neema yako tu Ni upendo wako tu Ni kwa neema yako tu Ni upendo wako tu Nakushukuru Mungu wangu Kwa yale yote umetenda Nakushukuru Mungu wangu Kwa mambo yote umetenda Huzuni yangu umeondoa Bwana Aibu yangu umeifuta Adui zangu umepigana nao Magonjwa yangu umeyaponya Acha nikushukuru Acha nikushukuru Asante, Asante Acha nikushukuru Acha nikushukuru Asante, Asante Asante, Asante Yesu Wewe ni Mwema Asante, Asante Yesu Wewe ni Mwema Asante, Asante Yesu Wewe ni Mwema Asante, Asante Yesu Wewe ni Mwema
Writer(s): Sara Nyongole Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out