Credits

PERFORMING ARTISTS
Darkid
Darkid
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Thabit Juma Thabit
Thabit Juma Thabit
Songwriter

Lyrics

[Verse 1]
Mi nataka tuzeeke wote
Nshakupenda sitaki uniache baby
Kamoyo chote nshakugea
Nishaacha mapepe nimetulia
[Verse 2]
Penzi lako kama niko peponi
Kama wewe sijaona dunian hii
Mahaba matamu najilia
Napewa bure sijalipia
[Verse 3]
Kila nachotaka unanipa
Sa nitoke kwako niende wapi mimi
Jeuri ya kukuacha ndo sina
Nakupenda hakuna kuachana
[Refrain]
Moyo wangu upo salama tangu nkupate
Nshateseka sana, sasa acha nnennepe
Ulikuwa wapi mama
Tumechelewa kukutana
[PreChorus]
Nimekufa nimeoza kwako nyang'a nyang'a
Wewe ndo mpenzi wangu mimi
Aki ya Mungu tena nimezama
Wewe ndo baby wangu mimi
[PreChorus]
Mwengine mwengine sina mimi
Wewe ndo tamu yangu mimi
Unantosha wewe tu jaman
Wewe usingizi wangu mimi
[Chorus]
Nipeni maiki nataka nimtangaze
Mpenzi wangu, mpenzi wangu
Simama laazizi wakuone
Mpenzi wangu, mpenzi wangu
[Chorus]
Jamani mmemuona
Mpenzi wangu, mpenzi wangu
Tunaendana aa
Mpenzi wangu, mpenzi wangu
[Verse 4]
Wanataka kulivunja hili penzi
Tunavyopendana eti hawapendi
Zidisha mahaba wateseke
Nigande usikwende popote
[Verse 5]
Waambie kwangu umefika mama
Hawawezi kutuachanisha baby
Penzi limeshaota mizizi
Haliwezi kufa kipuuzi
[Verse 6]
Mungu ndo kapanga tupendane
Na wakututenga ni yeye pekee
Mwanadamu nani wa kupinga
Hata waroge kigoma tanga
[Refrain]
Moyo wangu upo salama tangu nkupate
Nshateseka sana sasa acha nnennepe
Ulikuwa wapi mama
Tumechelewa kukutana
[PreChorus]
Nimekufa nimeoza kwako nyang'a nyang'a
Wewe ndo mpenzi wangu
Aki ya Mungu tena nimezama
Wewe ndo baby wangu mimi
[Chorus]
Mwengine mwengine sina mimi
Wewe ndo tamu yangu mimi
Unantosha wewe tu jaman
Wewe usingizi wangu mimi
[Chorus]
Nipeni maiki nataka nimtangaze
Mpenzi wangu, mpenzi wangu
Simama Lazizi wakuone
Mpenzi wangu, mpenzi wangu
[Chorus]
Jamani mmemuona
Mpenzi wangu, mpenzi wangu
Tunaendana aa
Mpenzi wangu, mpenzi wangu
[Outro]
Moyo wangu upo salama tangu nkupate
Nshateseka sana, sasa acha nnennepe
Ulikuwa wapi mama
Tumechelewa kukutana
Written by: Thabit Juma Thabit
instagramSharePathic_arrow_out

Loading...