Lyrics

Ohh Oh, ohh Salome juu ya kaburi lako nalia, haa! Kilio nakisikia Dakika za mwisho mpenzi wangu najutia, aah Kosa nilokufanyia Salome juu ya kaburi lako nalia, haa! Kilio nakisikia Dakika za mwisho mpenzi wangu najutia, aah Kosa nilokufanyia Siku ya kwanza nilikutana na wewe Akili iliruka na kupata kiwewe Sikuamini kama ningekutana na wewe Hilo la kwanza naomba unielewe Nikakutongoza ukanikubalia Ulijipa moyo tena mia kwa mia Umekwishapata bwana atakayekuoa Kumbe nilikuona kama demu wa kuzugia Miezi saba mbele iliendelea Na mapenzi kwako we' yakapungua Kumbe ulikuwa na mimba ya kujifungua Miezi yote hiyo wala hukuniambia Ulijua lazima nitaisaigia Na ndio ndoto yangu hiyo ilikuwa Na ulipojaribu mimi kuniambia Katukatu nami nikakutalia Salome mpenzi wangu ukaanza kulia Kwa uoga wangu mimi nikakuambia Tuonane siku inayofuatia Kwa unyonge Salome ukaitikia Salome juu ya kaburi lako nalia, haa! Kilio nakisikia Dakika za mwisho mpenzi wangu najutia, aah Kosa nilokufanyia Salome juu ya kaburi lako nalia, haa! Kilio nakisikia Dakika za mwisho mpenzi wangu najutia, aah Kosa nilokufanyia Siku ya pili tena ilipofikia Asubuhi mapema mi' nikakimbia Nikakimbia na kuelekea Mbeya Huku nyuma Salome uliningojea Saa, dakika, sekunde zilipotokea Ulichoka mpenzi kwa kuningojea Ikakubidi uje kuniulizia Nyumbani wakesema Dully ameshakimbia Salome mpenzi wangu ulinyong'onyea Hazikupita dakika ukazimia Ndoo za maji tatu wakakumwagia Ndipo hapo fahamu zikakurudia Ulilia mwishowe mpaka kujutia Ulijuta kwa nini ulikunikubalia Ulirudi nyumbani kwenu unalia Hadi chumbani kwako ukajifungia Salome mpenzi wangu ukaandika barua "Msimfunge Dully, mimi najiua" Dakika tano mbele zilipowadia Polepole kitanzi ukajifungia Ukajinyonga na kuiaga dunia Nisamehe Salome leo najutia Ukajinyonga na kuiaga dunia Nisamehe Salome leo najutia Salome juu ya kaburi lako nalia, haa! Kilio nakisikia Dakika za mwisho mpenzi wangu najutia, aah Kosa nilokufanyia Salome juu ya kaburi lako nalia, haa! Kilio nakisikia Dakika za mwisho mpenzi wangu najutia, aah Kosa nilokufanyia Salome juu ya kaburi lako nalia, haa! Kilio nakisikia Dakika za mwisho mpenzi wangu najutia, aah Kosa nilokufanyia Salome juu ya kaburi lako nalia, haa! Kilio nakisikia Dakika za mwisho mpenzi wangu najutia, aah Kosa nilokufanyia (Ha, Dully sykes, Mika Mwamba)
Writer(s): Dully Sykes Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out