Lyrics

Weka pombe sigara chini subiri tuongee Zima kijiti marijuana za nini? Ngoja tuongee Mbona ulisema mengi ukitaka nipotee Sa umefanya nini? Na ulisema nini wala usijitetee Macho hayana pazia Nilimwona navutia Naye kanikubalia Kumbe moyoni unaumia Dunia imejaa visanga Ubinadamu umekuwa majanga Tembo amefungwa kwa banda Anataka kula kuku pia na vifaranga Mungu tu akusamehe Wewe ni kama ndugu yangu Upunguze ma ugali Uadui wa nini mwenzangu we Ukitenda kosa na haujaomba radhi unakosea (Kosea) Mama yake mzazi huruma ungemwonea (Mwonea) Chunga kinywa kiwe na kituo Hekima ndo iwe funguo Maneno ya nini? Unajivua nguo Kumbuka ulimwengu ni kama chuo Ungenyamaza, kaa kimya Bora ungenyamaza kama huna la maaana Ungenyamaza, ukikosa heshima Bora ungenyamaza, bora kukaa kimya Ungenyamaza, bora ungenyamaza Bora ungenyamaza Ungenyamaza tu, bora ungenyamaza Kuwa muungwana Mmmmh hasira hasara Mimi ni ndugu yako kanitoa kafara Ukakesha hukutaka kulala Ukipambana niharibikiwe kaka wa Mtwara Ukasahau mapenzi ni siri Tena siri ya wawili Kilichokuponza maadili Tamaa ukashindwa isitiri Tunza heshima yako Na mashabiki zako wajivunge Na unapotongoza warembo Boxer usiweke pembeni Macho hayana pazia Nilimwona anavutia Naye kanikubalia Kumbe moyoni unaumia Ukitenda kosa na haujaomba radhi unakosea (Kosea) Mama yake mzazi huruma ungemwonea (Mwonea) Chunga kinywa kiwe na kituo Hekima ndo iwe funguo Maneno ya nini? Unajivua nguo Kumbuka ulimwengu ni kama chuo Ungenyamaza, kaa kimya Bora ungenyamaza kama huna la maaana Ungenyamaza, ukikosa heshima Bora ungenyamaza bora kukaa kimya Ungenyamaza, bora ungenyamaza Bora ungenyamaza Ungenyamaza tu, bora ungenyamaza Kuwa muungwana
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out