Lyrics

(Harmonize) Furaha isio kifani kukupata Mwandani hakika wamependeza Goma lipo uwanjani kaibiwa nani Sa unaachaje kucheza (Mpoto) Ama kweli harusi imefana tena ya ki historia Pande zote baba na mama naona Wanashangilia ila sitaki kua Mnafiki jumba bovu kuniangukia Nina langu moyoni Ningependa kuwaambia Bi harusi mashoga wa kukupia hao Ni wa kuwaangalia Wako wale u hali gani Wanakuja kuchungulia owaombe Samahani uwakomeshe wambea Eti wifi umepika nini na mimi utanigaia waambie Umepika dagaa zenye pili pili nyingi Zinakutosha wewe na na mme wako Wao watakimbia (Harmonize) Eeh aiii shemeji tubu ya mmeo Usikize ya fulani na hii ndo meseji Sema na mmeo usitafute ya jirani Kwa furaha niliyo nayo niacheni Nimwage radhi aiyoyoo Niacheni nimwage Radhi mi nataka nimwage radhi (Mpoto) Ng'ombe anapoita ndama tunasema Kwamba analia kupigwa na kulalama Hatujawahi kusikia hakika mmpendeza mi Navyomfahamu bi harusi Sipati kusimulia nimetokea Ruvuma chogolo,namtumbo lindi Mtwara mpaka chatoholi nimezisikia (Mpoto) Sifa binti huyu mola amemjalia Binti hapendi majungu hakika ni Nachowaambia ukimuazima viatu Na gauni anakuachia bwana harusi Tunakupa mke ukaishi naye vyema Nyumbani huna kitu husimfiche Mwambie tahadhari (Mpoto) Ikiwezekana mkakope mkono uende Kinywani husimpige mateke kisingizio Kitu fulani ohh umefanya nini Jana hakuliki mtoto bado mteke Usimkomaze kwa ngumi Ukishindwa mrudishe kwao hajaua huyu (Mpoto) Mmeo akienda kazini akirudi Salimia wala husikae chini chakula Kumsukumia mkaribishe ndani Hali ukimjulia muulize za kazini Kwa tabasamu muruaa Kisha msindikize bafuni ata kama anapajua Alafu wewe tafuta kiti jikoni kimbilia Simu yako meseji ukimtumia mwambie Bila wewe chakula hakitaingia (Harmonize) Eeh aiii shemeji tubu ya mmeo Usikize ya fulani na hii ndo meseji Sema na mmeo usitafute ya jirani Kwa furaha niliyo nayo niacheni Nimwage radhi aiyoyoo Niacheni nimwage Radhi mi nataka nimwage radhi (Mpoto) Nawaomba niishie hapaa taarishi Hua hafungwi naomba nichape lapa Yaliyobaki ni ya makungwi Niliowakera samhani kusema ni jukumu Langu nawaomba muishi kwa amani Hio ndio furaha yangu (Harmonize) Mmmh Ndoa ni kama safari Tuombeane dua atuepushe na shari Sa chini ya jua aah somo yake Mwari ainuke mama yake mwari Ainuke baba yake mwari ainuke Aje kati tulicheze ngoma kaka Yake mwari ainuke dada yake mwari Ainuke shangazi yake mwari ainuke Aje kati tulicheze ngoma (Harmonize) Niacheni nimwage radhi Mi nataka nimwage radhi Niacheni nimwage radhi Niacheni nimwage radhi Mi nataka nimwage radhi
Writer(s): Mrisho Mpoto Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out