album cover
Barua
40,314
Hip-Hop/Rap
Barua was released on June 16, 2000 by Sony Music Entertainment East Africa as a part of the album Kamanda
album cover
AlbumKamanda
Release DateJune 16, 2000
LabelSony Music Entertainment East Africa
Melodicness
Acousticness
Valence
Danceability
Energy
BPM90

Credits

PERFORMING ARTISTS
Daz Nundaz
Daz Nundaz
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Miikka Aleksanteri Kari (Miikka Mwamba)
Miikka Aleksanteri Kari (Miikka Mwamba)
Composer
Feruzi Mrisho Rehani (Ferouz)
Feruzi Mrisho Rehani (Ferouz)
Lyrics
David Celestine Jacob Nyika (Daz Baba)
David Celestine Jacob Nyika (Daz Baba)
Lyrics
Rusajo Israel (Sajo)
Rusajo Israel (Sajo)
Lyrics
Rashid Kaombwe
Rashid Kaombwe
Lyrics
Noel Kapinga (Critic)
Noel Kapinga (Critic)
Lyrics
PRODUCTION & ENGINEERING
Miikka Mwamba
Miikka Mwamba
Producer

Lyrics

Oya namna gani mzee?
Mbona leo upo hivi mzee?
Ah basi tu
Vipi mchizi wangu mbona naona kama umesizi
Unaonekana kama moyoni una majonzi
Au dili zako leo haziendi sawa?
Jinsi unavyoonekana kama umepagawa
Niambie ili nielewe
Ili na mie nisipagawe
Kwani tangu nimefika nakuona umepooza
Hebu niambie kitu gani unachowaza?
Sema basi nini kinacho kusumbua nafsi?
Niambie basi au kuna kitu kimekugasi?
Aah we bora acha tu wangu kachaa
Ni stori ndefu nikianza kukupa
Ubongo wangu nahisi kama unaanza athirika
Kwa haya matatizo makubwa yalonifika
Shemeji yako nadhani unamjua
Ambaye kichwa changu alikichengua
Baada ya kuishi muda mrefu na wangu lazizi
Nikabidi niende kuwataarifu wazazi
Kwamba nishampata mwenzangu ambaye ntafunga nae pingu za maisha
Na nlikuwa na hakika hakuna ambae atae tutenganisha
Basi bwana baada kurudi yangu safari
Nkakuta mlango wa geto umepigwa kufuri
Nauliza watu wote sipati jibu
Ni mkasa mkubwa mwenzako ulonisibu
Nikaanza lisaka tunda langu kwa sana
Lakini jitihada mwisho zikashindikana
Nikaamua basi mi kutulizana
Nikawa sitoki nje nipo ndani tu nalala
Huku mawazo mengi kichwani yamenitawala
Katika mahaba tulishazama dimbwini
Lakini barua niliyopokea nashindwa hata kuamini
Ua la moyo wangu halipo tena na mimi
Barua hii jamani inanihuzunisha
Kila nsomapo moyo wangu unasononeka
Na ufukara ndo uliotutenganisha
Subiri basi story nikumalizie
Enhe
Mkasa huu mwanangu ulionifika mie
Enhe
Hususani imepita wiki kadhaa, ndipo hapo nikapokea barua
Kilichokuwa ndani sikukitambua
Nikaja kuelewa baada ya kuifungua
Nikakuta barua yenye ujumbe mzito
Ikiwa imeambatana na kadi ya mwaliko
Ndege wangu ameruka hayupo tena nami
Sasa hivi sijui mwenzangu mimi nani
Hali yangu duni imenifanya kuelemewa
Na hivi karibuni demu wangu anaolewa
Barua inanisisitiza Harusini nihudhurie
Sijui siku hiyo hata wapi mi nianziee
Mpenzi umeniacha kwenye nyavu nimenasa
Nimebaki kama kipofu sioni pa kupapasa
Nikisoma barua hii kumalizia huwa nashindwa
Kwani nahisi kama hivyo nishadunda
Shika mwenyewe usome barua hii
Soma mwenyewe uone barua hii
Shika mwenyewe usome barua hii
Soma mwenyewe uone barua hii
Ikufikie wangu wa enzi mpenzi
Mi kiafya mzima, natumai na we kiafya u hai
Dhumuni la barua ni kukutaka na wewe kujua nini hasa na kipi kisa na mkasa
Kilichonishawishi mbali nawe kwenda kuishi
Sio siri mimi binafsi kupenda kuishi maisha duni ya chini sana
Kumbuka ufukara umasikini kututenga vimechangia ila usipinge bwana
Sasa nani alaumiwe unadhani
Hivi punde tu nataraji kufunga pingu maishani ili niishi maisha ya thamani
Yaliyo gharama tena adimu kama Almasi
Fanya hima usikose harusini ukipata nafasi
Katika barua hii nimeambatanisha kadi hii ya mwaliko ni yako
Basi usimalizie kusoma, Basi usimalizie kusoma
Kwaniukiendelea moyo wangu unauchoma
Kwa kuondoka wangu huyu mpenzi
Moyo wangu umejawa na simanzi, niliamini nitatenganishwa na umauti
Sasa nimekubali fukara hana sauti
Mola ndiye anayegawa umasikini na utajiri
Naye hali yangu mpenzi ameshindwa kuihimili
Na ndio maana unaniona leo nimeshika tama
Ni sawa na kifaranga aliyekosa mama
Aliyemgaia yeye ndie aliyenipa mimi ufukara
Lakini naamini ipo siku nyota yangu itang'ara
Katika mahaba tulishazama dimbwini
Lakini barua niliyopokea nashindwa hata kuamini
Ua la moyo wangu halipo tena na mimi
Barua hii jamani inanihuzunisha
Kila nsomapo moyo wangu unasononeka
Na ufukara ndio ulotutenganisha
Katika mahaba tulishazama dimbwini
Lakini barua niliyopokea nashindwa hata kuamini
Ua la moyo wangu halipotena na mimi
Barua hii jamani inanihuzunisha
Kila nsomapo moyo wangu unasononeka
Na ufukara ndio ulotutenganisha
Written by: David Celestine Jacob Nyika (Daz Baba), Daz Nundaz, Feruzi Mrisho Rehani (Ferouz), Miikka Aleksanteri Kari (Miikka Mwamba), Noel Kapinga (Critic), Rashid Kaombwe, Rusajo Israel (Sajo)
instagramSharePathic_arrow_out􀆄 copy􀐅􀋲

Loading...