album cover
My Muna
album cover
00:00
03:35
00:00
04:22
Past 7 Days
My Muna was discovered most frequently in the first few seconds of the song during the past week

Music Video

Music Video

Lyrics

[Intro]
Mai Maimuna
My baby Maimuna
Mai wewe Mai wewe mhh
[Verse 1]
Ati kumbe unapenda ninavyolia
Ati kumbe unapenda ninavyoumia
Ati kumbe kweli navyosikia
Eti kama nikifa msibani hutohudhuria
Moyo wangu
Sio wa chuma ni wa nyama
Mbona umeuchoma sana
Nimejitahidi niweze kusahau ya nyuma
Ila nahisi imeshindikana
Mwili wangu
Mifupa mama
Nakonda nakonda sana
Ungesubiri tuwakuze wana
Umeondoka mapema sana
Naumia
[PreChorus]
Nilichokukosea ni kipi Maimuna
Mbona unanisusia watoto hutaki kuwaona
Kama upo mbali mi nauli nitatuma
Rudi tafadhali nipate japo afya njema
[Chorus]
Oooh nasononeka
Nasoneneka hata nikifa ujue ni wewe
Ooh oh oh nateseka
Nateseka hata nikifa ujue ni wewe
Mai unanivuruga
Nasononeka hata nikifa ujue ni wewe
Mai unanichanganya sana sana
Nateseka hata nikifa ujue ni wewe
[Verse 2]
Zilipita dakika yakaja na masaa
Siku zimekatika sasa unafika mwaka
Bado nakukumbuka moyoni hujatoka
Kama unanisikia rudi nyumbani sasa
Sili silali chakula kinywani hakipiti
Basi jibu hata message maana simu haushiki
Dhoofu ilhali nayasubiri tu mauti
Mkwezi mwenye mnazi leo nimekalia kuti
[PreChorus]
Nilichokukosea ni kipi Maimuna
Mbona unanisusia watoto hutaki kuwaona
Kama upo mbali mi nauli nitatuma
Rudi tafadhali nipate japo afya njema
[Chorus]
Oooh nasononeka
Nasononeka hata nikifa ujue ni wewe
Ooh oh oh nateseka
Nateseka hata nikifa ujue ni wewe
Mai unanivuruga
Nasoneneka hata nikifa ujue ni wewe
Mai unanichanganya sana sana
Nateseka hata nikifa ujue ni wewe
[Outro]
Oooh Mai Maimuna
Oooh Mai Maimuna
Rudi nyumbani Mai wangu
Maimuna
Watoto wanakusubiri
Maimuna
Written by: Aslay
instagramSharePathic_arrow_out􀆄 copy􀐅􀋲

Loading...