album cover
Kapeperuka
album cover
00:00
01:20
01:35
01:50
03:35
00:00
03:51
Past 7 Days
Kapeperuka was discovered most frequently at around 1 minutes and 35 seconds into the song during the past week

Music Video

Music Video

Lyrics

[Verse 1]
Nililifuma penzi kwa uzi wa chuma
Japo sina kucha alipowashwa nilimkuna
Kuna muda aliumwa hospitali ugonjwa hawakuona
Nikafuata waganga Moro Tanga na Kigoma akapona
Akapona yeye
Nilifubaa nilichakaa kusudi asije lala na njaa
Na nilifanya mpaka kang'aa
Waliomcheka walimshangaa
[PreChorus]
Kapata mabawa karuka matawi kindege
Kabeba hadi ndala sasa chooni naendaje
Nilijua nitakula mwenyewe chakula nilichopika
Kumbe nilijenga barabara kila mtu anapita
Kasuku uko wapi wewe
Niliyekuita malaika
Mi nilijuaga masihara kumbe ndo unaniponyoka umekwenda
[Chorus]
Kapeperuka kapeperuka
Kaniachia maua kapeperuka
Kapeperuka kipepeo
Kapeperuka kapeperuka
Taabani naugua
Kapeperuka kapeperuka
[Verse 2]
Angesema mapema singejisumbua
Ningemwacha afe tu wakati anaugua
Nilipoteza muda wangu kumtibia
Kwa kujua atakuwa wangu eti kanikimbia
Nasikia anakula ananenepa
Mwenzake nalia lia nimebaki mifupa
Jamaa naugua naugua
Niliye mtegemea jamani kanitupa
Wanasema cha mtu mavi ukikiona kitemee mate
Ila cha kwangu asali wamekitafuna kwa mkate
[PreChorus]
Kapata mabawa karuka matawi kindege
Kabeba hadi ndala sasa chooni naendaje
Nilijua nitakula mwenyewe chakula nilichopika
Kumbe nilijenga barabara kila mtu anapita
Kasuku uko wapi wewe
Niliyekuita malaika
Mi nilijuaga masihara kumbe ndo unaniponyoka umekwenda
[Chorus]
Kapeperuka kapeperuka
Kaniachia maua kapeperuka
Kapeperuka kipepeo
Kapeperuka kapeperuka
Taabani naugua
Kapeperuka kapeperuka
Written by: Aslay
instagramSharePathic_arrow_out􀆄 copy􀐅􀋲

Loading...