Texty

Inafaa kunena Inafaa kunena labda ni muhimu sijui Labda kusimulia si karama kama wanavyosema Ikiwa msimuliaji huingia hatarini Labda kweli baraka ni laana njema Wasikilizaji nasikia wana ndoto na wenyewe Si uongo Hadithi nzuri ndo' kilele kwa wasikilizaji Ila ndoto ya msimuliaji Ndoto ya msimuliaji ni kulindwa milele Kwanini azibwe mdomo wakati ubongo unapiga kelele? Si lazima msimuliaji apazwe la hasha! Atandikiwe majani au aandikwe kama mwanasiasa Lakini lengo lake awe huru msimuliaji atambe Alindwe ili waovu waonyeswe, mashujaa watangazwe Ona kuna wasimuliaji hukwepa pande tupu Yani baada ya mitaji husimulia upande wa wenye nguvu Wapo wabinafsi wanaotangaza jinsi asili ilivyowahusudu Husimulia walivyoshinda vita wakigombea asali na wadudu Swali ni je? Nani atasimulia hadithi ya wadudu? Nani atasimulia kua si mara zote mchukua asali alimsulubu mdudu? Nani atasimulia hadithi ya shetani, Baada ya kusikia upande wa Mungu? Baada ya kusikia upande wa Mungu Waungwana kumbukeni ya muhimu na ziada Kumbukeni ya uchumi jamii na siasa Lindeni ghala la chakula na maji Lakini msisahau kumlinda msimuliaji, ni afya Japo kuwa msimuliaji si alama ya taifa Lakini fikiria mtu ambaye yupo tayari kulipa gharama ya maisha Msimuliaji hukukumbusha ulipotoka ujue unapoenda Na hiyo ndio faida Labda ukumbuke ya mdimu na majoka Au simulizi za mizimu ya mloka Au tarihi ambazo ni historia za kuziheshimu Maana asiyeijua historia, huweza kurudia makosa Msimuliaji hachagui upande maana hapendi kupotoka Hafungamani na misalaba au alama za mwezi na nyota Alama za wasimuliaji walioidondosha kheri Waliookota sifa wakati wakiidondosha kweli Enyi wa khaki kijani na manjano Mmeona nyekundu ile pale? Haijaja pale leo ipo tangu kale Msiruhusu iwaguse Si kwakua hamna hadhi La hasha Ila ile rangi anaifahamu msimuliaji Ile rangi ni damu iliyomtoka au kumrukia Na mchanganyiko wa pande zote za dunia Anaijua leo, aliijua jana Hajaisoma au kuisikia Aliipata wakati akitafuta vya kusimulia Na ni hivi anavyotaka kukusimulia leo Nyakati za katikati kwenye eneo la ukanda wa kidachi Zilizaliwa lugha tatu, Lugha ghafi Na kati yao ilikuwepo lugha iliyoitwa lugha ya watu Kwenye ukanda huu msimuliaji Hakuitwa Narrator au story teller kwa kiingereza Hakuitwa Erzahler japo kuwa ukanda huu Ulikuwa karibu sana na Ujerumani Hakuitwa Rawi kwakua huu ukanda haukuwa wa kiarabu Msimuliaji aliitwa the Verteller Kama Christopher Hitchens Ama Professor Laurence Krauss Ama Shaaban Robert Ama Francis Scott Key Fitzgerald Ama Chimamanda Ngozi Ama Fred Saganda Ama Alice Walker Ama Octavia Burtler Ama Lufufu Mkandala Ama Rainfred Masako Dizasta vina, mabibi na mabwana Ni the Verteller
Writer(s): Edger Mwaipeta Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out