Lyrics

Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje Wewe umetangaza pumziko la kweli kwamba wote wenye mizigo waitue kwako kama sio wewe mwokozi kutupumzisha mizigo yetu tungeitua wapi Tena umetanga kwa wenye magonjwa kwamba kwa kupigwa kwako wote wamepona kama usingejitoa kupigwa mtini wenye magonjwa wangeponywa na nani Tena umesema na wote wenye kilio kwamba siku moja watanyamazishwa kama usingeyaona machozi ya wengi nani angeweza kujinyamazisha mwenyewe(Asante) Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje Hata kwa walioshushwa chini wewe upo unamwinua mnyonge kutoka chini Unakichagua kionekacho dhaifu ili upate kukiabisha chenye nguvu Hata katika shida tunazopitia umesema yesu hautotuacha maana mkono wako si mfupi hata usiweze kututoa kwenye tabu Ni kweli tunapita kwenye misukosuko lakini tunajua yesu wetu upo nasi maana umesema ni heri wenye huzuni siku yao ipo watafarijika Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje Hata kwa wasio na baba wewe upo umesema nikuite baba kama usingeuona ukiwa wangu ni nani leo ningemwita baba Hata kwa mama yangu nimekuona umemvusha katika ujane wa tabu kwa misukosuko mingi aliyopitia bila wewe yesu asingeliweza Wewe ni mungu utabaki kuwa mungu unatuwazia mawazo yaliyo mema ungekuwa mwingi wa ghadhabu kwa wanadamu ni nani leo hii angesimama Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje Bonus Kuna wakati wa kulia wakati wa kuombeleza wakati wa kusema mungu wangu mbona umeniacha Maana hakuna wakati mgumu kama wakati wa shida hata ndugu yako wa damu atajitenga nawe Utasema labda mpendwa mwenzangu atanisaidia hata mpendwa mwenzio atajitenga nawe Utasema labda mpendwa mwenzangu atanisaidia hata mpendwa mwenzio atajitenga nawe Nimejifunza kwamba wakati wa matatizo hata yule aliyekupenda anajitenga nawe maana hata wakati wa yesu...
Writer(s): Martha Mwaipaja Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out