Lyrics

Kujisikia nipo juu mie sitaki hizo deals Sipendi makuu hivyo nitabaki kuwa real Na kila track ya Q aaah,. Ni wazi utaifeel Ni wazi iko full aah mzazi ninakill Ninamwagika kama Masika. Ninaheshimika na sio kanjibai Kwa huu mziki wa bajaji Hadi kwa washkaji wenye macadillac Unawashika ile kibabylon Unauzika sana maghetoni Ilimradi tu wawe happy more Midadi tu ila party no Mkisinzia mtaniudhi nishawapa vyeo Tuwape wapuuzi waliodai hii haiuzi haya matokeo Safari ni hatua, kufika inabidi uianze Haina kukita au kusita, inabidi ukaze Ingia, ongoza au fuata njia, kukimbia ni mwiko Kuanzia ulipo sio sawa na kubakia ulipo Nikisema 'chini hapana' nina maana fanya unyanyuke Na ukiamini umesimama mwana. Komaa usianguke Ukijituma na neema inakaribia Nyuma walio-give up mapema wangekaza wangeifikia Penye... Happy, jitusu, unafki usiuruhusu Yajue ya kuzingatia ili uachane na yasiyokuhusu Kibongobongo longolongo shazi Endelea kusaka mchongo hata ukipata kazi Tunachukiana? Ndio. Ila sio sababu kuacha riadha ya mafanikio Ongeza mbio Sababu kila mtu, kila kona anasaka mafanikio Haukungoji wakati. Ooh wewe Zinapita nyakati.ooh wewe Muda wako bahati. Oh wewe Na kughairisha kisa haupati sapoti Ni kujificha na kuuliza giza Iko wapi ile tochi? Haupati ile noti Na wakati wa ule uboss ushapotea Hautaki ukose? usiache ofcoz endelea Utafanikiwa kwa unachojua au unachofanya Wachache ndio hutusua kwa jinsi tu wanavyoonekana Mafanikio hayaji ukikata tamaa Yenyewe huwafuata wanaojituma Na wale wasiosukumwa na njaa Sipigi kila dili mipaka imezingatiwa Sitaki kuwa tajiri ninataka kufanikiwa Ili kuheshimiwa kwanza ni lazima ujiheshimu Lakini kufanikiwa ni maujanja tu sio lazima elimu Ili kuyadaka wengine hugeuka wabaya Mafanikio kwenye kuyasaka wengine hugeuka malaya Hugeuka was(i)o haya Kutwa utawakuta kwa babu Na anayefanya mambo ya maana Huwa hana muda wa kuyahesabu Kwenye kuyasaka hakikisha haufilisiki Haupotezi maisha au vile vitu havinunuliki Sio kama hatucheki kwasababu tumezeeka? Nope,ni tunazeeka kwasababu hatujawahi cheka Tunachukiana? Ndio. Ila sio sababu kuacha riadha ya mafanikio Ongeza mbio Sababu kila mtu, kila kona anasaka mafanikio Haukungoji wakati. Ooh wewe Zinapita nyakati.ooh wewe Muda wako bahati. Oh wewe Utumie basi... Eeeh eeeh Una mpenzi (na) uko lonely? Im sorry ndugu. Haujafanikiwa Maisha ni kama boli, magoli ndio kufanikiwa Oooh ooh oooh.oooh. Ndio kufanikiwa Kila mtu anataka mafanikio... Hhhmmm. Hhhhmmm. Oh mafanikio Oh mafanikio Kila mtu anataka mafanikio
Writer(s): Fareed Kubanda Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out