Music Video
Music Video
Credits
PERFORMING ARTISTS
Obby Alpha
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Obby Alpha
Songwriter
Lyrics
Angalau hawajajua udhaifu wangu
Maana wangejua Mbona ningeteseka
Angalau hawajajua sura yangu ya huzuni
Maana wangejua hawa wangenitesa
Kama wangejua nikikosa pesa nahangaika
Kama wangejua hawa wangenitesa
Au kama angejua kiukweli nampenda
Kama angejua mbona angenitesa
Bridge
Hivyo sitafanya vitu vya kufurahisha
Ulimwengu mzima maana sitoweza
Bali nitafanya vitu vya kuutikisa
Ufalme wa Bwana na kumfurahisha
Chorus
Angalau angalau, Angalau hawajajua udhaifu wangu
Angalau angalau, Angalau hawajajua udhaifu wangu
Hivi mi nawaza wangejua matatizo yangu
Kiukweli wangenisumbua kisa shida zangu
Au wangejua ninavyompenda Mungu
Wangesambaza kanisani majungu
Au kama wangejua mimi kwenye giza sioni
Wangenisumbua kunipaka tope usoni
Ahsante Mungu wangu umewatia upofu hao
Hata madhambi yangu umeyafanya ni sisri kwako
Maana Tabasamu langu limekuwa ni chukizo kwao
Ila we ukanipenda Mungu na ukanifanya Mwana wako
Hivyo sitafanya vitu vya kufurahisha
Ulimwengu mzima maana sitoweza
Bali nitafanya vitu vya kuutikisa
Ufalme wa Bwana na kumfurahisha
Angalau angalau, Angalau hawajajua udhaifu wangu
Angalau angalau, Angalau hawajajua udhaifu wangu
Hivi kaam wangejua nikikosa pesa naangaika angalau hawajajua udhaifu Wangu
Au kama angejua kiukweli nampenda, Angalau hawajajua udhaifu wangu
Written by: Obby Alpha