Music Video

Pastor
Watch {trackName} music video by {artistName}

Featured In

Credits

PERFORMING ARTISTS
Roma Mkatoliki
Roma Mkatoliki
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Roma Mkatoliki
Roma Mkatoliki
Songwriter
Ibrahim Musa
Ibrahim Musa
Composer

Lyrics

Yeah! Wacheni watoto wadogo waje kwangu Maana ufalme wa Mbinguni ni wao J. Rider where you are I'm the pastor of this church I'm the pastor of this church I'm the-, it's Tongwe Records Fanya ishara ya msalaba, upokee haya mahubiri Mimi ni mteule, ninawaletea injili Nina ushuhuda wa kiroho, Bwana yuaja msubiri Natangaza upako, na habari za mnara wa Babeli Wachungaji wanalumbana wakigombania waumini Wanalala (wanalala), wakiamka wanaanzisha dini Hawaogopi damu ya msalaba, Bible wanaifanya biashara We siyo Yesu hatakama baba yako fundi seremala We' ni nani usokosea kila unayemuombea anapona? Hatutaki shuda za uongo, aminini nyote mtachomwa Ndani ya vazi la suti, unakebehi wakatoliki Mtaleta dini zote ila R.C itabaki Hata Kristo alipoponya hakutaka malipo Account yako imejaa sadaka zetu wakristo Toba yako haijaswihi halafu unajiita una upako Sio kila ata'yenita bwana basi ataiona pepo We' ni nani unayejiita nabii kwenye jamii? Hizi nyakati za mwisho, soon atashuka Masihi Piga magoti tusali (amen) Piga magoti tusali (amen) Waumini wamekimbia kanisa, madhehebu yanaongezeka Hizi nyakati za mwisho, check manabii wa uongo! Mwana wa Adam yuaja (amen) Mwana wa Adam yuaja (amen) Laiti ningeweza, ningekugeuza jiwe la chumvi Vipi unipangie sadaka? Pastor gani? We mlanguzi Hakika ili neno, "Usitumikie mabwana wawili" Siasa na kanisa kama hadithi za Cain na Abel Ka' wasabato was'okula kitimoto wala kambare Wanasadiki mbele ya haki, wanaamini agano la kale Mnatangaza ufahari wenu kwenye vikapu cha sadaka Hakuna sadaka ya kweli kama kumchinja Isaka Kanisa lako halifanani na ufalme wa Jehova Madhehebu yanajitenga kama makundi ya bongo fleva Heshima ya mkatoliki, inashuka kama theluji Dini mmeifanya miradi kwa kivuli cha uchungaji Kanisani mnaonyeshana, ufahali wa kuvaa bazeee Hekalu mnalichafua kwa sadaka ya pedeshee Biblia hujaimaliza unataka uzima wa milele Usije ukatuchoma moto ka' wafuasi wa Kibwetele We' ni nani unayejiita nabii kwenye jamii? Hizi nyakati za mwisho, soon atashuka Masihi Piga magoti tusali (amen) Piga magoti tusali (amen) Waumini wamekimbia kanisa, madhehebu yanaongezeka Hizi nyakati za mwisho, check manabii wa uongo! Mwana wa Adam yuaja (amen) Mwana wa Adam yuaja (amen) Hizi nyakati za mwisho, soon atashuka Masihi Wewe una mamlaka gani mpaka unajiita nabii Kukataza waumini wasivae mapambo kwako jadi Ili pesa wakupe sadaka na kisha unafanya mtaji We' mchungaji umekusanya waumini kwenye vijiji Ukawaongoza sala ya toba kama Yohanna mbatizaji Unabeba gunia la zambi, na Yesu kumvika taji Usini'ekee mkono kichwani huna karama ya uponyaji Imani yako ndogo kama punje ya aradani Uza mali zako zote pesa uwape maskini Si unatupa kiini macho unatumia gari ya kanisa Halelluya halelluya, kumbe unatuibia sadaka Yesu hakuwa mganga wa kienyeji japo alimponya kipofu Kwa tope la mate yake ila kwako napata hofu Eeh, Mungu napiga goti hiki kikombe kiniepuke Mwana wa adamu yuaja basi tungoje ashuke We' ni nani unayejiita nabii kwenye jamii? Hizi nyakati za mwisho, soon atashuka Masihi Piga magoti tusali (amen) Piga magoti tusali (amen) Waumini wamekimbia kanisa, madhehebu yanaongezeka Hizi nyakati za mwisho, check manabii wa uongo Mwana wa Adam yuaja (amen) Mwana wa Adam yuaja (amen) "Angalieni mtu asiwadanganye Maana wengi watakuja kwa jina langu wakisema mimi ni Kristo Nao watadanganya wengi", halellujah (ameen) "Manabii wengi wa uwongo watatokea Kutakuwa na dhiki kubwa siku hiyo Je hamsadiki ya kuwa hizi ni ishara kwamba mwana wa adam yuaja?" (Amen) "Basi kesheni mkisali maana hamjui saa wala siku" I'm the pastor of this church I'm the pastor of this church I'm the-, it's Tongwe Records
Writer(s): Ibrahim Musa Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out