Lyrics

Yahwéh! Nainua macho nitazame pande zote Nione kama yupo wa kumweleza shida zangu Naona hakuna wote wamepungukiwa Hawana furaha, hawana matumaini Nakumbuka habari za yule mwanamke Aliyetokwa damu miaka kumi na miwili Aliposikia kwamba Yesu anapita, aliazimia akasema moyoni mwake Nitajisogeza mpaka nifike kwa Yesu, nitajisogeza mbele ya umati wa watu Nitajipenyeza mpaka nifike kwa Yesu, niguse pindo lake ili nipate uzima Akajisogeza mpaka kafika kwa Yesu, akagusa pindo lake mara akawa mzima, akapona Nami Bwana ni sawa na yule mwanamke, aliyetokwa damu miaka kumi na miwili Nimeshasikia habari za matendo yako Nimeazimia nami Bwana moyoni mwangu, nitahakikisha mpaka nifike kwako Yesu Niguse pindo lako kansa iniondokee Niguse pindo lako umasikini ukae mbali nami Nimechoka kuonewa mimi namtaka Yesu Nasema sikubali kufa na magonjwa yangu Nitajisogeza mpaka nifike kwa Yesu, nipone Kuna watu wengine jamani wananishangaza Unapowaambia habari za kumwona Yesu Wanaanza kuuliza eti unatoka wapi Wananisahangaza na maswali ya ajabu Unatokea wapi, kanisa lako ni lipi? Nasema nipisheni, mimi namtaka Yesu Maswali sitaki, mimi namtaka Yesu Nimweleze shida zangu ili nipate kupona Nimweleze shida zangu ili nipate amani Nisikie furaha nipate kuburudika moyoni Kwa habari ya dhambi huyu Yesu alishinda Aliposhuka kuzimu mbona ilinyamaza kimya Alikanyaga kifo nayo mauti ilimezwa Akatoka yu hai sasa Yesu yuko mbinguni Anatawala mbinguni anamiliki duniani Acheni huyu Yesu jamani aitwe Mungu Acheni huyu Yesu jamani aitwe Mungu milele Nimechoka kuonewa mimi namtaka Yesu Nimechoka kuonewa, mimi namtaka Yesu Nimweleze shida zangu taabu ziniondokee Nasema sitaki, mimi namtaka Yesu Namtaka Yesu nipone (Yule bwana wa mabwana) Namtaka Yesu nipone (Yesu ni Mungu wa huruma) Namtaka Yesu nipone (yeye ni baba wa yatima) Namtaka Yesu nipone (Yesu ni mume wa wajane) Namtaka Yesu nipone (Nasema fitina sitaki) Namtaka Yesu nipone (jamani majungu sitaki) Namtaka Yesu nipone (nasema nimechoka kuonewa) Namtaka Yesu nipone (aah) Namtaka Yesu nipone (mimi majungu sitaki) Namtaka Yesu nipone (marafiki wabaya sitaki, eeh) Namtaka Yesu nipone (wenye fitina siwataki)
Writer(s): Maureen Nkirote Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out