Lyrics

Haya yaya yaa yaaa yaangu Eeeh Jipange sawasawa Unatoka wapi unakwenda wapi Unatoka wapi unakwenda wapi Je wajua majira na nyakati unazoishi sasa Unawaza nini unajifunza nini Unawaza nini wajifunza nini Je hujui ya kwamba maisha yako yamefika mwishoo Najua unatamani kua tajiri wa kwanza dunia nzimaa Lakini hufikirii kua wa kwanza mbinguni kwenye uzimaa (weee) Najua unatamani kwenda Amerika kusini najua hiloo Lakini hujatamani kwenda kwa Mungu mbinguni hatari hiloo Mwenzangu unatamani kupata maisha mazuri Kwa raha zako Lakini hufikirii kujua ni nini hatima ya roho yako (wee) Naona una hangaika kwa hali na Mali kutaka umaarufu Lakini hufikirii kuhangaika kupata utakatifu Mbona unaona fahari kupika majungu wengine wahangamie Lakini hufikirii kunena maneno ya Mungu waokolewe Pole pole mama Pole pole mama Shetani anakutamani pole mama Hujui unaloliwaza pole mama Shetani anakutamani pole mama Kiburi kinakudanganya pole mama Unadhani Mungu amechanganyikiwa kama wewe polee Hukumu iko palepale kiama iko palepale Jehanamu iko palepale mauti iko palepale Hukumu itachukua mkondo wake na wewe umekwisha Tabasamu la mamba kufurahi kuona mawindo Tumia akili yako vizuri Wee simama jipange sawasawa Simama jipange sawasawa Simama jipange sawasawa Simama jipange sawasawa Je filosofia ya Mungu Kwa habari ya hukumu ya dhambi Na ule ufufuo wa wafu ndio kusema umepitwa na wakati Aaah uuoo ni upumbavu wa mwanadamu na ujinga wake (wee) Mawazo ya Mungu ni thabiti akili zake hazichunguziki Teknolojia yake iko juu sanaa imeshinda zote Pole pole mama Pole pole mama Shetani anakudanganya pole mama Shetani anawinda roho yako pole mama Ni heri ungelijua pole mama Ungempa Yesu maisha yako pole mama Tabasamu la mamba kufurahi kuona mawindo Tumia akili yako vizuri Wee simama jipange sawasawa Tumia akili yako vizuri na ujue linalokupasa Shetani anakutamani wee simama jipange sawasawa Tumia akili yako vizuri na ujue linalokupasa Shetani anakutamani wee simama jipange sawasawa Macho yako mbele funga mkanda songa mbele Simama kiumee jipange sawasawa Macho yako mbele hatua kumi songa mbele Simama kiumee jipange sawasawa (weee) Haiyaa iyaa iyaaa Oooh iyaaa iyaaa Eeeh Simama jipange sawasawa (Shetani anakudanganya mama) Simama jipange sawasawa (Shetani anawinda roho yako mama) Simama jipange sawasawa (Shetani anataka roho yako Baba Simama jipange sawasawa (Usimkubalie mama) Wewe jipange sawasawa (Rudi rudi rudi) Wewe jipange sawasawa (na Yesu anakutamani) Wewe jipange sawasawa (dunia isikudanganye Baba) Wewe jipange sawasawa (dunia inakudanganya Baba) Haaaiya iiyaaa aaah Hakuna jipya chini ya jua (wewe jipange sawasawa) Yesu anakuja na ujira mkononi (wewe jipange sawasawa) Yesu anakuja na ujira mkononi (wewe jipange sawasawa) Haaaiya iiyaaa aaah (wewe jipange sawasawa)
Writer(s): Maureen Nkirote Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out