Similar Songs
Credits
PERFORMING ARTISTS
Mercy Masika
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Mercy Masika
Songwriter
Lyrics
Baba nichukue, nifunze, nataka kusoma,
Kwa shule yako, kwa shule yako
Nichukue, nifunze, nataka kusoma,
Kwa shuke yako, kwa shule yako.
Nikiwa nawe kama mwalimu,
Ninajua nitahitimu,
Nitashinda adui akileta majaribu,
Unitayarishe, unibadilishe,
Mtihani nipite, mwito nilipize,
Nijue kuandika, niandike maono yangu,
Nijue kuhesabu, nihesabu baraka zako,
Nijue kuongea, nihubiri neno lako,
Kwa watu wako.
Baba nichukue, nifunze, nataka kusoma,
Kwa shule yako, kwa shule yako
Nichukue, nifunze, nataka kusoma,
Kwa shule yako, kwa shule yako.
Shule yako hatudanganyi, ni ukweli na uwazi,
Wanafunzi hawagomi, mwalimu atujali,
Unifunze mipango, wote niwaheshimu,
Yesu ni mwalimu, yesu ni mwalimu,
Nijue kuandika, niandike maono yangu,
Nijue kuhesabu, nihesabu baraka zako,
Nijue kuongea, nihubiri neno lako,
Kwa watu wako.
Baba nichukue, nifunze, nataka kusoma,
Kwa shule yako, kwa shule yako
Nichukue, nifunze, nataka kusoma,
Kwa shule yako, kwa shule yako.
(THE END)
Writer(s): Mercy Masika
Lyrics powered by www.musixmatch.com