Lyrics

Ulianza wewe, wakaja waimbaji na wabana pua Wale mwewe, Franga wawindaji wakatusua Kwakuwa, wanajua mshikaji unaishi kwa miko Na zako itikadi, ziko kimziki na sio mshiko Kama haileti hela, basi haimake sense, No sweat kisela mie nikakomaa tu na lako penzi Sikusound garbage au kuchange suddenly Mie ni mjeshi so naweza fight savagely Hiphop ya ukweli, Ikapigwa radioni Malaika wa kheri nao hutembelea motoni Penzi ni kipofu na anayemuona halioni Sikuwa na hofu, mama alinipenda tangu nikiwa tumboni I started young, I made my mother's womb a drum My umblirical chord a guitar, muhoji aliyenizaa Bongo Flava mzuri kiasi, hiphop we ndo my queen My 1st my last & everything in between Mimi na wewe, tangu long time Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame Chaajabu hujabadilika na uko Mwenye main stream Bongo Hiphop Bongo Hiphop Mimi na wewe, tangu long time Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame Chaajabu hujabadilika na uko Mwenye main stream Bongo Hiphop Bongo Hiphop Kama kukupenda wewe ni dhambi, basi shetani yu nami Na kamwe sintonyea kambi ili niwabambe dukani For a million little pieces naweza kumcon Oprah ka James Frey Na watasema sitishi wakati wanaogopa nisitokee Waufuate mkumbo huu wa wasomi, wa midundo na mistari Ukiwa na nyundo mkononi, ni rahisi kupigilia msumari Sio tu bongo, mpaka Ng'ambo hakuna uhuru wa habari Kuna uhuru wa mwenye chombo, mitambo na mwenye mali Kujifanya hawasikii, haiwasaidii, wala haiwajengi Unachosema ni, kamwe IPP haitompinga Mengi Unawakumbusha wazazi wa uswazi, chati ya uteja imeingia Na Mapusha wanauza drugs ili walishe familia Mbaya, kuhifadhi fuvu la mtu ndani ya kabati Mbaya zaidi ni kuwa na ndugu, halafu kichwa maji Amka bongo lala, hiphop sio ufala, ni lazima uifate Uaminifu ni kama mshahara, fanya kazi ili uupate Mimi na wewe, tangu long time Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream Bongo Hiphop Bongo Hiphop Mimi na wewe, tangu long time Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame Chaajabu hujabadilika na uko Mwenye main stream Bongo Hiphop Bongo Hiphop Mapenzi ya sikuhizi, bila kugombana yanakua hayana stimu Pia ni ruksa kushikana lakini sio kushikiana simu Inanipa wazimu, kusikia kimwana haujaachana na Hasheem Na bado mnawasiliana, una mpango wa kuchanganya timu? Nakupenda hiphop, ndo maana ninarap ile mbaya Naspit fire bila hennessy, au kula kaya I want my art to be my legacy, kabla sijaretire, Waanze nigwaya hawa enemies Anyways ni hayo tu Beef huletwa na wivu na wivu sio hiphop MC nayetaka beef amlete Maza ake kwa strip club Bongo flava ananipima kama nimeiva kimasomo Anagundua mie ni dreamer pia ni believer zaidi ya Common Cha ajabu hunitempt ili nikuache hip hop Anaahidi atanipa good sex wewe unanipa true lover Hajui who's next. wewe unanipa tu mashavu Nikipaa. anaumia. anatamani nishuke chini Nami sikutamani ustaa Ustaa ulinitamani mimi Nilichohitaji ni kuitumia hii sanaa ili nishee na nyinyi Hii zawadi. niliyopewa na mpaji ninayemuamini Mpaji aliyenivika taji ilimradi incharge ni win Na ninaamini kuna muda huongea kwa kupitia mimi Na hunisamehe ninapokosea. ni vyema mkanizoea nyinyi Naweza kuona unachotaka au atakachonionyesha Nikitoa ngoma wanaitaka wanaipata Coz wewe ni special Mimi na wewe, tangu long time Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream Bongo Hiphop Bongo Hiphop Mimi na wewe, tangu long time Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream Bongo Hiphop Bongo Hiphop
Writer(s): Fareed Kubanda Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out