Lyrics

Woi woi woiee... nenda Tenda wema nenda zako... nenda Usingoje kusifiwa mama wee Usisubiri asante ...nenda Usingoje shukrani mama wee.nenda Wanadamu si wema mama wee Wana meno wanauma mama wee Wanawasha kama pilipili mama wee Wanaupupu utajikuna wee mama Meno yao kama chumaaa... mama wee Tenda wema nenda zako utalipwa na Mungu Ukisubiri kusifiwa mama we Ukingoja shukurani mama wee.mama Makubwa yatakukuta mwenzangu wee Makubwa yatakukuta pole we Matusi utayasikia pole wee Dhihaka utazitambua mama wee Kachiba utatupiwa mama wee Tenda wema nenda zako mama Nasema usigeuke nyuma ...nenda mama Nenda... nasema nenda... aaah nenda utalipwa na Mungu Siku ya mateso yako pole wee Siku ya mateso yako mama wee pole wee Siku ya huzuni yako mama Siku ya mahangaiko yako mama we Siku ya anguko lako mama wee... pole wee Waliokuwa rafiki zako mama Watageuka mwiba kwako polee Waliokula chakula chako mama Watageuka anguko laako mama wee polee Uliotenda wema kwao pole wee Yatageuka maumivu yako polee Waliokula chakula chako... siku ile Watasahau wema wako mwenzangu wee Watakaa vibarazani jamani eee Watacheka na vicheko mama wee Majina watakupatia pole wee Tena mabaya yenye hatia tena Mabaya yenye udhia kwako Watakuita kimbelembele kimbelembele Ati wewe kimbelembele mwenzangu kimbelembele Wema wako kimbelembele kimbelembele Uliwasaidia kimbelembele kimbelembele Uliwasaidia kimbelembele ati wewe kimbelembele Mama mama... mama wee mama mama Usichoke kutenda mema utalipwa na Mungu Wacha niseme ukweli jamani ee Wacha niseme ukweli mwenzangu wee Wanadamu hawabebeki hawabebeki Hata ukifanya nyinyi hawabebeki Wabebe kwa mbeleko ya chuma... hawabebeki Wabebe kwa maturubai .hawabebeki Watachukua na viwembe jama ee mama Watachana turubai kweli Wachane wakukimbie pole wee Wabebe kwa mbeleko ya chuma hawabebeki Watatafuta misumari jama ee mama Watagonga ngo ngongo ngongo ngongo Wape chakula wale haya washibe wakutukane jama ee mama Wape chakula wale tena kesho watakushitaki mama wee Nenda nenda... aah nenda utalipwa na Mungu(uuuuuu) Mukama kwange kwagara kwagara Mwami wanje kwagara kwagara Mukama kwange kwagara nyo kwagara Omukwano kwagara kwagara Mama mama wee... mama mama wee mama Tenda wema nenda zako utalipwa na Mungu(uuuu)
Writer(s): Maureen Nkirote Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out