Lyrics

(Mmh) ah leo Chereko chereko chereko mwanenu nimekuaa Zile kuringa mideko itapunguaa Asante Mama ulinifunza nkajuaa Baba kasema kuomba mwiko Raha ya chumvi kununua Tena si kwa nazi si hirizi za waganga Kwa Baraka za baba na mama tunaduaa Mwambie paparazi pingamizi wenye viranga Walosema hayawihayawi yamekua (Oh oooooh) Iyena iyena iyena iyena iyena iyena Kwaheri tutaonana Iyena iyena iyena iyena iyena iyena Ntawakumbuka sana Ooooh ndoa baraka ukipata ushukuru Mana wanoililia ni wengi sana Kwa watoa talaka kuitoa ni kufuru Nimefunzwa vumilia uushinde ujana Ili kesho mahususi kusudi wasinong'one Embu nichumu niringe washushuke Na hii pete ya harusi nakuvisha waone Wakale sumu wavimbe wapasuke Ah tena shika nanga nteke nisichomoke ndani(anameremeta) Futa namba wablock vimada wa zamani(anameremeta) Sio vijembe vya kanga wazi wazi mambo hadharani(anameremeta) Hio walopanga mwenye nyumba kaja ndani(anameremeta) Iyena iyena iyena iyena iyena iyena Kwaheri tutaonana Iyena iyena iyena iyena iyena iyena Ntawakumbuka sana Imefika tamati tulisubiri kitambo Leo samaki kanasa kwenye chambo Pongezi kwa kamati yanavutia mapambo Napata picha safi litanikoma bando Mwanamke usafii gaga kulisugua Mume akirudi sharti viatu kumvua Kitandani marashi massage kumchua Kisha anzasayansi viuno kutengua Mambo ya kuzima taa si mahaba ni kuwanga Washa japo ka mshumaa mumeo aone shanga (Yii) make-up kinanda kakasuti kama mbunge (anameremeta) Mulochanga muda kujipoza na punje (anameremeta) Humo ndani shivo amekuja na fumbwe (anameremeta) Kula chanda ukishiba ruksa kafunge (anameremeta) Iyena iyena iyena iyena iyena iyena Kwaheri tutaonana (kwaheri baba mama) Iyena iyena iyena iyena iyena iyena Ntawakumbuka sana Sa nataka kusasambua (sasambu) Mi nasasambua (sasambu) Midadi na sasambua mi (sasambu sasambua tuone) Mguu mmoja juu (sasambu) Usishushe chini (sasambu) Cheza jitazame (sasambu sasambua tuone) Aisha kimobiteli (sasambu) Nipe za baloteli(sasambu) Nyonga kibaskeli(sasambu sasambua tuone) Aka kama unashika ukuta (sasambu) Jifanye unasusa (sasambu) Taratibu zungusha(sasambu sasambua tuonee) Sasambu Sasambu Sasambu Sasambua tuonee Kama unawasha bajaji(sasambu) Imwagie na maji(sasambu) Tuwakomeshe (sasambu sasambua tuone)
Writer(s): Nasibu Abdul Juma Issaack, Raymond Shaban Mwakyusa Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out