Music Video

02-Bahati Bukuku - Ni nyakati za mwisho
Watch {trackName} music video by {artistName}

Credits

PERFORMING ARTISTS
Bahati Bukuku
Bahati Bukuku
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Bahati Bukuku
Bahati Bukuku
Songwriter

Lyrics

Ni nyakati za mwisho wee Jamani njooni tumuombe Mungu Yeye atusaidie maana ni siku za mwisho Ni nyakati za mwisho Tanzania tumuombe Mungu Maana gonjwa la ukimwi linaitikisa dunia Taifa tumuombe Mungu eeh Yeye atusadie maana vitendo vya ugaidi vinaitikisa dunia Hebu fikiria ajali ya Dodoma ilivyomaliza watu, hilo naomba ujue Hebu fikiria gonjwa la ukimwi linavyomaliza watu, hilo naomba uzuru Hebu fikiria tena naomba kumbuka vitendo vya ugaidi vilivyomaliza Hivi wewe na mimi Tunapoyaona hayo tunajifunza nini kutoka kwa hao wenzetu Au tunasubiri sala za marehemu wawaite wachungaji waje kutuombea Je maisha yako wewe, nani atayadhamini usipomruhusu huyu Yesu Yeye kufanyta marekebisho Elimu yako kaka, nani ataidhamini usipomruhusu huyu Yesu Yeye kufanya marekebisho Ujana wako wewe, nani ataudhamini usipomruhusu huyu Yesu Yeye kufanya marekebisho Kinachonitia uchungu ninapowaona wapendwa wanangangania dini Wanamkataa huyu Yesu Kinachonitia uchungu ninapowaona wapendwa wanangangania vyeo Wanamkataa huyu Yesu Ukifa leo wewe nani atakudhamini usipomruhusu huyu Yesu Yeye kufanya marekebisho Vyeo vyako baba nani atavidhamini usipomruhusu huyu Yesu Yeye kufanya marekebisho Uongozi wako Baba nani ataudhamini usipomruhusu huyu Yesu Yeye kufanya marekebisho Maisha yako wewe nani atakayedhamini usipomruhuus huyu Yesu Yeye kufanya marekebisho Au unafurahishwa na yale majina ya wafu wakuite maiti wakuite marehemu Wakuite hayati wakuite msiba au inapendeza yeye aje akusaidie Lakini maisha yako leo nani atakudhamini usipomruhusu huyu Yesu Yeye kufanya marekebisho Ukifa wewe leo nani atakudhamini usipomruhusu huyu Yesu Yeye kufanya marekebisho Maisha yangu mimi, nani angenidhamini asingekua ni huyu Yesu Yeye kufanya marekebisho Maisha yangu yote, nani angenidhamini asingekua ni huyu Yesu Yeye kufanya marekebisho Minakushukuru Mungu, kwa upendo wako huo Kuniokoa maisha yangu, ningekua wapi mimi? Minakushukuru Mungu, kwa upendo wako huo Kugharamia maisha yangu, ningekua wapi mimi? Maisha yangu mimi nani angenidhamini, asingekua ni huyu Yesu Yeye kufanya marekebisho Usomi wako wewe, nani ataudhamini, usipomruhusu huyu Yesu Yeye kufanya marekebisho Usomi wako kaka, nani ataudhamini, usipomruhusu huyu Yesu Yeye kufanya marekebisho Mpokee Yesu leo, yeye katika maisha yako Awe bwana na Mokonzi ili afanye marekebisho Mpokee Yesu leo katika maisha yako Awe bwana na mokonzi yeye afanye marekebisho Mpokee Yesu leo
Writer(s): Kelvin Kioko Bahati Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out