Lyrics

Baba nichukue, nifunze, nataka kusoma, Kwa shule yako, kwa shule yako Nichukue, nifunze, nataka kusoma, Kwa shuke yako, kwa shule yako. Nikiwa nawe kama mwalimu, Ninajua nitahitimu, Nitashinda adui akileta majaribu, Unitayarishe, unibadilishe, Mtihani nipite, mwito nilipize, Nijue kuandika, niandike maono yangu, Nijue kuhesabu, nihesabu baraka zako, Nijue kuongea, nihubiri neno lako, Kwa watu wako. Baba nichukue, nifunze, nataka kusoma, Kwa shule yako, kwa shule yako Nichukue, nifunze, nataka kusoma, Kwa shule yako, kwa shule yako. Shule yako hatudanganyi, ni ukweli na uwazi, Wanafunzi hawagomi, mwalimu atujali, Unifunze mipango, wote niwaheshimu, Yesu ni mwalimu, yesu ni mwalimu, Nijue kuandika, niandike maono yangu, Nijue kuhesabu, nihesabu baraka zako, Nijue kuongea, nihubiri neno lako, Kwa watu wako. Baba nichukue, nifunze, nataka kusoma, Kwa shule yako, kwa shule yako Nichukue, nifunze, nataka kusoma, Kwa shule yako, kwa shule yako. (THE END)
Writer(s): Mercy Masika Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out